Tuesday, August 17, 2021

FAHAMU NINI MAANA YA NEBULA

Nebula ni Mavumbi Vumbi ya Mawingu yenye gesi ya Hydrogen na Helium pia yaliyo na ( Atom,molecule au Substance ) ambayo yanapatikana Ukanda wa Interstellar Space ...

Nebula Ni Mchakato wa mwanzo kabisa katika Maisha ya Nyota nyingi sana Hizi tuzionazo . michakato hii mingi hutapata kuiona kama Utaichunguza zaidi Milkyway na mbali zaidi kuendelea kwa Jinsi vile Ulimwengu wetu Unavyotanuka .... Bubble Nebula Au NGC 7653

Katika Picha za Hapo Juu Tunapata Kuiona Moja ya Picha ikionesha Moja ya Mchakato wa Nebula ambayo iliyopewa Jina la Bubble Nebula nadhani Hii ni kutokana na Muonekano wake ulivyokaa kama Puto ... Nebula Hii iligunduliwa na Kupigwa Picha Na wanaanga wa NASA/ESA Kwa kutumia Hubble Space Telescope ambapo iliweza Kuivuta Umbali wa 8000 light years away .... Bado wanaanga Hao wanaendelea Kuifuatilia ili waweze kuona hatua kwa hatua Hadi Mwisho wake ....

Meleezo Kutoka Kwa Moudy

Posted on August 17, 2021 | Categories:

Saturday, August 14, 2021

JE BINADAMU WALITOKEA WAPI ( KISAYANSI )

BINADAM WALITOKA WAPI? SEHEMU YA KWANZA

Ni swali lililoulizwa na rajabu karimu huku akitaka majibu ambayo yapo kisayansi zaidi Sasa swali hilo ni gumu kidogo na itabidi niandike gazeti sababu ili tuweze kupata majibu basi lazima history ihusike, geography, ihusike, biology ihisike, chemistry ihusike na hiyo dini ambayo haitaki tuitumie hapa nayo itabidi ihusike ili tujulishane kwanini dini haitaki tuitumie hapa

Nimepata wakati mgumu katika kutafakari kwamba nianzie wapi Ila at least nitaanzia kwenye kuzaliwa kwa sayari yetu ya dunia mpaka kutokea kwa binadam nadhani hapo tutakuwa tume cover eneo kubwa na kujifunza zaidi

Sasa ktk makala hii msingi Mkubwa utaegemea katika nadharia iitwayo "organic evolution theory" ambayo ndo nadharia inayokubalika katika sayansi Ila pia tutaangazia kuhusu chimbuko la uhai in general Sasa mfumo nitakaotumia kuandika makala hii ni "mfumo rejea" nadhani wale wataalam Wa kiswahili tutakuwa pamoja (mfumo huo ni ule Wa kuchanganya mbele Kati nyuma) Sasa tukianza na asili ya uhai tunaweza kujiuliza uhai ulitoka wapi? Nini chanzo au chimbuko la uhai?

Swali hili limekuwa likiulizwa miaka nenda miaka rudi na kutafutiwa majibu ambyo mpaka sasa yapo katika nadharia 5

1)Special creation theory(uumbaji maalumu) Nadhria hii inasema kuwa chanzo cha uhai na kila kitu katika ulimwengu viliumbwa na nafsi kuu ya asili ijulikanayo Kama Mungu nadhaia hii inaungwa mkono na dini nyingi zikiwemo uislam na ukristo kwa imani yangu Mimi ya ukristo(nadharia hiyo inaelezewa katika kitabu cha mwanzo 1:1, injili ya yohana Mt. 1:1-18) katika bibilia takatifu tunaambiwa Mungu aliumba ulimwengu na kila kitu kwa muda Wa siku 6 na siku ya 7 akaitakasa akapumzika Mwaka 1665 askofu aliyejulikana kwa jina la James usher alijaribu kupiga hesabu kuona ni lini tukio la uumbaji lilifanyika? Alichokifanya alikuwa akijumlisha miaka ya uzao Wa yesu kurudi nyuma mpaka kuja kumkuta Adam (uzao Wa yesu umeelezewa katika injili ya mathayo Mt. 1 na kuendelea) na hivyo alikuja kugundua kuwa ulimwengu uliumbwa miaka 4004 BC na uumbaji ulianza mwezi Wa kumi tarehe 1 na kukamilika tarehe 23 ya mwezi huo Huo saa tatu kamili asubuhi, na hii ndo imepelekea waumini wengi Wa dini(hasa wasabato) waamini ulimwengu una umri Wa miaka 6000 sababu tangu yesu apae mbinguni imepita miaka 2000 + sasa ukijumlisha na ile miaka 4004 utapata miaka 6000+ lakini askofu usher anakuwa kinyume na maandiko matakatifu sababu kwa mujibu Wa mahesabu yake tunaona tukio la uumbaji limechukua siku 22 wakati bibilia inasema uumbaji ulifanyika kwa siku 6 tu

Sasa tukirudi katika sayansi tunaona kuwa sayansi inadili na "observable phenomena" Kama nilivyoelezea katika makala ya "From what is physics to the theory of everything" kuhusu mbinu tatu za kusoma sayansi ambazo ni observation, measurement na practicals sasa katika uumbaji huo hakuna mtu aliyeshuhudia tukio la uumbaji likifanyika na hapo ndipo sayansi inapotilia shaka kuhusu nadharia hii na kizuri kuhusu sayansi ni kwamba katika sayansi huwa hatujiulizi kuwa Mungu alitoka wapi sababu antambulika kama "supernatural being" sasa Kama kuna neno nature ndani maana yake swali hilo linakuwa halina maana na kingine ni kwamba sayansi haiingiliani na maswala ya kiimani japo mwanasayansi mmoja mmoja anakuwa na dini anayoiamini mfano ni Isaac newton alikuwa mkristo mmoja safi kabisa na alifanya kazi nyingi katika dini kuliko tunavyomjua katika upande Wa sayansi aliweza hadi kupiga hesabu kiama kitakuwa lini na kwa Mara ya kwanza alipata jibu kuwa kiama kitakuwa mwaka 2016 Ila aliporudia mahesabu yake alikuja kupata 2060 kwahiyo tusubiri(time no matter what will tell) ingawa katika bibilia tunaambiwa hakuna anayejua siku ya kiama hata yesu hajui isipokuwa Mungu baba tu, pia newton anweza akawa sahihi kuhusu mwaka Ila siku na saa ndo hajui (who knows?) Sasa mwanasayansi Wa kwanza kuikosoa nadharia hii ya "special creation theory" ni Aristotle ambaye alizaliwa huko ugiriki mwaka 384 BC na kufariki mwaka 322BC Huyu alipinga kwa kutumia utafiti na hivyo utafiti wake ulipelekea ipatikane nadharia ya Pili inayojulikana Kama spontenous generation theory

2)spontenous generation theory Nadharia hii inasema kuwa uhai ulitoka katika viumbe visivyo hai na alipata ushhidi huo kwa kuona chawa wanatokea endapo nguo itakuwa chafu, au nyama inaoza na kutoa funza hivyo chawa na funza ni viumbe hai ambao tutasema wametoka katika vitu visivyo hai kwani uongo? Sasa miaka ya 1600 mwanasayansi Fransisco redi alifanya utafiti kwa kuchukua nyama mbili moja akaiacha wazi na nyingine akaifunga kabisa katika mazingira ambayo sio rafiki kwa kitu chochote kugusana nacho na baada ya siku kadhaa alikuja kukuta ile nyama aliyoiacha wazi imeoza, inatoa funza na ile ambayo aliifunga vizuri alikuta haijaharibika ndipo akagundua kuwa Aristotle hakuwa sahihi na kile tulichokiona nyama kutoa funza ni kwasababu ya viumbe wadogo wadoo wasioonekana kwa macho walikuwa huwa wanajishikiza na kuozesha kitu mfano ni bacteria pia wadudu kama nzi wanaweza kuacha mayai yao hapo na yanapokuja kuanguliwa ndipo tunaona funza Sasa jaribio kama hilo lilikuja kufanywa tena na mwanasayansi Lazaro spallanzani miaka ya 1700s na kupata matokeo yale Yale mam aliyoyapata mtangulizi wake Fransisco redi Na ugunduzi huo ulipelekea tupate tekinolojia iitwayo "biotechnology"ambayo hutumiwa viwandani katika kuzalishia vitu kama pombe kwa kutumia viumbe wadogo wadogo(mfano fangasi aitwae yeast hutumika kutengenezea pombe pia hutumiwa katika kuumua maandazi katika mchakato uitwao fermentation ambapo yeast huchakata kiwango fulani cha wanga na kuunda pombe na gesi ya carbon dioxide ambayo huumua ngano na kufanya ivimbe Ila pia wengine huitumia migahawani kwa kuchanganya kwenye unga Wa ugali sababu unga wa ugali bado ni wanga na kuufanya uumuke na kutoa ugali Mkubwa hivyo inawapa faida kimtindo) Nadharia ya tatu inaitwa cosmozoan theory

3)Cosmozoan theory Nadharia hii inasema kuwa uhai ulitoka huko katika magimba mengine na kuja kufika hapa duniani kwa njia mbali mbali ikiwemo ya kushuka kwa vimondo sasa ukakasi Wa nadharia hii ni kwamba mpaka sasa hatujapata ushahidi Wa uwepo Wa viumbe hai nje ya dunia kuanzia mercury mpaka Pluto hakuna ambapo tumeona angalau kuna chembechembe za ushhidi Wa viumbe hai au hata kuonesha kuwa kulikuwaga na viumbe hai labda tusubiri majibu ya vifaa vilivyorushwa katika sayari ya mars tuone vitatupa majibu gani nadharia ya nne

4)Steady state theory Nadharia hii inasema kuwa kila kitu unachokiona katika ulimwengu ikiwemo na viumbe hai vilikuwepogo tu havina mwanzo wala nini Lakini ukakasi Wa nadharia hii ni kwamba katika kanuni ya ulimwengu iitwayo "law of causality au law of cause and effect" tunaona haiwezekani kitu kiwepo bila kuwa na chanzo chake basi huenda tukaitetea kwa kusema kuwa kuna "uncaused cause" na kubaki hapo na hivyo itaonekana Kuwa sahihi (who knows) ingawa nadharia hii kisayansi ilikuja kupingwa vikali na utafiti uliofanya na mwanadini george lematre miaka ya 1920s kutoka ubeligiji ambaye alipelekea kupatikana kwa nadharia ya "big bang"

Muendelezo wa Sehemu zinazofuata Utazikuta Kule Juu kwenye sehemu ya mada

Maelezo kutoka kwa Mwana astrophysikia Ndugu Archimedes Justine.

JE BINADAMU WALITOKEA WAPI.

SEHEMU YA PILI

Katika sehemu hii ya pili tutajikita zaidi kuiangazia sayansi inasemaje kufatana na mwendelezo Wa sehemu ya kwanza(ikumbukwe kuwa movie bado hijaanza hii yote ni trela) Sasa katika upande Wa sayansi tunarudi pale katika upande Wa "special creation theory" kwanza katika sehemu ya kwanza tuliona kuwa sayansi inpata ukakasi kuhusu nadharia hii kwasababu hakuna aliyeshuhudia tukio la uumbaji sio?

Lakini pia kifo cha waaminio kuhusu umri Wa ulimwengu kuwa ni miaka 6000 kilikuja mnamo miaka ya 1940s ambacho kililetwa na mwasayansi prof. Willard F Libby ambaye alikuja na ugunduzi Wa "carbon 14 isotope dating" ugunduzi huo ulimfanya apate tuzo ya Nobel Carbon 14 dating ni kipimo cha muda Wa mabaki ya viumbe walioishi miaka mingi iliyopita ili kujua waliishi lini sasa kwa vipimo vya mabaki mengi ya mifupa viliweza kuonesha kuwa viumbe wengi waliishi miaka mingi Sana iliyopita zaidi ya hiyo elfu sita mfano ni lile fuvu la mtu Wa kale lililookotwa pale Olduvai Georgi na Dr. Leakey mwaka 1954 Kama sikosei na kuonesha kuwa kiumbe hicho chenye fuvu hilo kiliishi miaka million tatu iliyopita(yani tukirudi nyuma miaka million tatu ndo tunakutana naye akiwa anaishi Kama time travel ingewezekana) Sasa carbon 14 dating inafanyaje kazi?

Tukirudi katika kemia tunajifunza kuhusu "organic compounds" kuwa karibu robo tatu ya vitu vyote duniani ni organic compound, organic compound ni jumla ya vitu vyote vyenye carbon atom ndani yake isipokuwa vitu vichache Kama carbon monoxide, carbon dioxide, hydrogen carbonate ions na carbonate ions,.... Sasa kwakuwa vitu vingi vina carbon element hapa tunaona haja ya kuiangazia carbon Kama carbon Carbon ni element ambayo inakuwa na idadi ya punje chanya(protons) 6 na electron 6 Ila tukija katika upande Wa uzito wake tunaona uzito Wa atom yoyote kwa asilimia 99 Unatokana na kiini chake ambako katika kiini huwa kuna punje chanya(protons) na punje zisizo na chaji(neutrons) sasa kwa carbon habari ya idadi ya neutrons inakua tofauti kidogo

1) kuna carbon zenye neutron 6 ambazo huunda jumla ya neutron na proton kuwa 12 sababu idadi ya proton hubaki vile vile 2)kuna carbon zenye neutron 7 na hivyo kiini chake huwa na jumla ya punje 13 3) kuna carbon zenye neutron 8 ambazo kiini chke huwa na jumla ya punje 14 Sasa aina ya kwanza ndo hupatikana kwa wingi katika ulimwengu takribani asilimia 99 na aina ya pili huchukua karibu asilimia moja yote kwahiyo aina ya tatu ipo katika ulimwengu Ila kwa kiwango kidogo Na aina zote tatu hujulikana Kama "isotopes za carbon" wakati kite do hicho cha atoms hizo Kuwa na idadi sawa ya proton huku zikitofautiana neutron huitwa "isotopy" na kwanini hutofautiana idadi ya neutron? Hiyo ni fizikia ya ndani Sana ambayo nisingependa niiangazie hapa Ila tutajifunzia kule kwenye makala ya "From what is physics to the theory of everything" Sasa hiyo aina tatu ambayo inapunje 14 ndo tunaiita carbon 14 na hii hupatikana katika viumbe hai mfano kwenye mifupa Sasa hiyo carbon 14 ni radioactive maana yake inakuwa inavunjika kuunda vipande viwili kwa kutoa punje zenye chaji hasi na kupelekea iundwe nitrogen kila baada ya miaka 5730(muda huo ambao kitu kitatumia kuvunjika vipande viwili huitwa half life) sasa hapo kuna kanuni inayotumika kukokotoa muda ambao kiumbe kiliikuwepogo miaka mingi kanuni hiyo ni N=Noe^-T(1/2)t

Katika kanuni hiyo N inamaanisha kiasi cha carbon kilichobaki No kiwango cha awali cha carbon T(1/2) ni half life t ni muda ambao hicho kiumbe kiliishigi Kwahiyo kwa kupima kiwango cha carbon 14 kichobaki katika masalia ya mifupa kisha unalinganisha na kiwango cha carbon 14 katika kiumbe kilichopo kinachofanana nae basi unaweza kuingiza katika kanuni hiyo na kukokotoa " t" hivi ndivyo carbon 14 dating inavyofanya kazi na kwa kupima masalia ya viumbe mbali mbali tumeweza kugundua kuwa dunia na ulimwengu kiujumla Una zaidi ya miaka 6000 hivyo concept hiyo ya kidini kuhusu umri Wa ulimwengu kuwa na miaka 6000 tupa nje ya dirisha Tukirudi kwenye nadharia zetu, katika sehemu ya kwanza tuliangalia nadharia nne sio? Sasa nadharia ya tano ni 5)Biochemical evolution theory Hii ni nadharia ambayo inakúbali kamiongoni mwa jamii ya wanasayansi ambayo yenyewe inasema kuwa chanzo cha uhai ni kutoka katika muunganiko Wa kemikali mbali mbali kama vile methane, ammonia, hydrogen na water vapour ambazo ziliungana by chance na kuunda amino acids ambazo ndo kiini cha viumbe hai wote

Nadhria hii ilipendekezwa miaka ya 1920s na mnamo miaka ya 1950smwanasayansi aitwae miller aliifanyia jaribio na jaribio hilo linaitwa "miller experiment" ambapo alichukua gesi ya ammonia, hydrogen, methane na water vapour akaweka katika mtungi maalumu maabara na kuupitishia "strong electric field" iliyopelekea zitokee cheche ambzo zilisababisha gesi hizo zijiunge ktk namna Fulani na kuunda amino acid ambazo kwa kupitia by chance zinaweza kuungana na element zingine kama phosphorous nk na kuunda vinasaba/genetic materials ambazo ni DNA(deoxyribonucleic acid) na RNA(ribonucleic acid) NOTE(tunaposema by chance tunamaanisha mam zari/probability mfano chukulia umempa tumbili computer atakavyokuwa anabonyeza bonyeza keyboard obviously atakuwa anaandika utumbo tu sio? Ila inaweza kutoa kama zali tu akijikuta kaandika neno moja lenye mantiki hata "Archimedes" sasa hivyo ndivyo ilivyotokea katika namna ya kupatikana kwa amino acid na safari mbele mpaka kutokea kwa viumbe hai)

Kipengele ambacho tutaenda kukijadili baada ya kufahamu hayo ni "organic evolution theory" Hiyo ni nadharia ambayo inasema kuwa viumbe vyote vimetoka sehemu moja Ila vilikuwa vikipitia mabadiliko Mdogo Mdogo kadri muda ulivyozidi kusonga mbele na hivyo kutufanya tutofautiane Sasa kabla sijaichimba hii nadharia kiundani nataka nikupe hints za ushahidi juu ya nadharia hii ili kuondoa utata ambao unaweza kujitokeza huko mbele 1)fossils remains(masalia ya viumbe hai) 2)comperative anatomy 3)cooperative physiology 4)comparative embryology 5)Number of chromosomes Kwa Leo tuishie hapo kipindi kijacho tutazidadavua kiundani hizo hints ambazo ndo ushahidi Wa organic evolution theory kisha tutaichimba organic evolution theory yenyewe

Maelezo na Archimedes Justine

JE BINADAMU WALITOKEA WAPI.

SEHEMU YA TATU

Katika sehemu ya kwanza tulijifunza kuhusu maana ya "organic evolution theory" sasa Leo katika sehemu ya tatu tutaangalia ushahidi Wa kisayansi kuhusu nadharia hii ya organic evolution

1)Masalia ya viumbe hai(fossils remains) Viumbe hai vinapokufa huoza sababu vinachakatwa na viumbe wadogo wadogo Kama bacteria na kupelekea kutoa baadhi ya elements katika mfumo Wa gesi Kama carbon dioxide, ammonia, hydrogen sulphide na kupelekea tuhisi harufu Sasa kuna baadhi ya viumbe unakuta wanashindikana kuoza sababu sio woote watakaooza mfano katika maeneo yenye baridi Kali huko viumbe kuoza ni kazi kidogo sasa tukirudi nyuma miaka mingi Sana takribani million 750 tunakutana na viumbe waitwao dinosaurs ambao walikuwa katika aina mbali mbali lakini sio hao tu pia miti mingi iliyokuwepo enzi hizo ambao kwa pamoja walikufa na wengine kuoza lakini wengine hawakuoza Sasa wale ambao hawakuoza walikuwa wanatitia chini kadri muda unavyozidi kwenda(unaweza ukashuhidia hili iache nyumba yako baada ya muda mrefu hata miaka 10 utaikuta Kama kimo chake kimepungua) sababu malighafi hititia chini sasa huko chini hufunikwa na miamba tabaka(sedimentary rocks) na kadri miaka inavyokwenda ndivyo viumbe walivyokuwa wakifa na kutitia chini huku wakikandamizwa na layers za miamba tabaka na kupelekea alama za miili yao kujichora katika miamba hiyo huku composition zao zikibadilishwa na kuwa mafuta ghafi, au gesi asilia au makaa ya mawe ambayo ndo tunayachimba Leo

Sasa kwa tafiti zilizofanyika katika alama za miamba kwa kulinganisha layers kutokea ya juu na kushuka hadi chini wataalam Wa miamba na wanabiolojia wameweza kuona kuwa alama za miamba iliyoko tabaka la juu hifanana na baadhi ya viumbe hai wanaoishi Leo wakati kadri unavyoshuka chini mfanano unazidi kutofautiana kutoka tabaka moja hadi jingine sasa hapo ndipo wakapata ushahidi kwamba evolution ilitokea sababu tunaona mabadiliko ya miundo Wa alama za viumbe kulingana na layers za miamba lakini pia kwa kupima masalia ya carbon 14 elements wataalam Wa kemia na miamba wameweza kujua miaka ya zama ambazo viumbe hao waliishi

2)Comparative embryology Huu ushahidi unazungumzia mfanano Wa vijusi vya viumbe mbalibali Wana baiolojia kwa kuchunguza vijusi vya viumbe mbali mbali pale vinapokuwa vinaundwa wameona vikifanana yani kijusi cha Kobe, samaki, binadamu, simba, kangaroo kuku nk vinafanana Sasa wakajiuliza kwanini inakuwa hivyo? Bila Shaka ni ushahidi tosha kuwa zamani sisi sote tulitoka katika chimbuko moja Ila tulikuwa tukipitia mabadiliko mbali mbali kadri miaka ilivyokuwa inakwenda

3)comparative anatomy Kwanza tujue anatomy ni nini? Anatomy ni muundo Wa mfumo Wa kiumbe hai bila kuangazia kazi zake Sasa ukiangalia viumbe wengi unakuta baadhi ya structure/muundo Wa organ zao zinakuwa zinafanana fanana mfano ukiangalia moyo Wa amphibia labda tuchukulie samaki, ukalinganisha na moyo Wa reptilia mfano mjusi na ukalinganisha na moyo Wa binadamu utaona kimuundo kuna utofauti Mdogo Moyo Wa samaki una vyumba 2 Wa reptilia una vyumba 3 wakati Wa binadam Una vyumba 4 huo ni ushahidi kuwa sisi sote tulitoka sehemu moja isipokuwa tulikuwa tukipitia mabadiliko kadha Wa kadha(evolution)

4) comparative physiology Physiology ni elimu inayoangazia kazi za mifumo ya kiumbe hai Sasa hapa kuna namna mbili ¡)Analogous structure Hii inaelezea kuwa baadhi ya viumbe huwa na organs ambazo kazi zinafanana lakini huwenda zikawa zinaonekana kutoka katika vyanzo mbali mbali mfano ni popo na kuku wote wanamabawa kwa ajili ya kupaa Ila wametofautiana chimbuko hii inaonesha kuwa mazingira yalichagiza kuwapelekea wao wawe na sifa hiyo ¡¡)homologous structure Hii inaelezea kuwa baadhi ya viumbe huwa na organs zinazofanana Ila hutofautiana katika kazi mfano ni nyani na binadam wote wana miguu ya mbele Ila kwa binadam hutumia kwa ajili ya kushikia vitu wakati nyani hutumia kwa ajili ya kutembelea

5)comparative chromosomes Hii inaelezea kuwa idadi ya chromosome hufanana fanana baina ya viumbe hai mfano binadamu Ana idadi ya chromosomes 46 wakati sokwe Ana idadi ya chromosomes 48 lakini pia muundo Wa hizo chromosomes unafanana fanana baina ya viumbe hai sasa ukaribu huo unaonesha kuwa sisi sote tumetoka katika chimbuko moja isipokuwa tulikuwa tukipitia mabadiko (evolution) kadri muda ulivyosonga Sasa chromosomes ni nini? Tutakuja kulijadili siku nyingine katika movie kamili maana trela yetu ndo inaishia hapo ingawa niliwahi kugusia kidogo chromosome ni nini katika makala ya "From what is physics to the theory of everything"

Maelezo na Archimedes Justine.

JE BINADAMU ALITOKEA WAPI.

SEHEMU YA 4.

Katika sehemu ya 1 mpaka ya 3 ilikuwa ni utangulizi ili tupate picha na mwanga katika kuangazia ufumbuzi Wa swali hilo kupitia sayansi ANGALIZO: 1)Hapa mjadala upo kisayansi zaidi, concepts zote za nadharia ya chimbuko la uhai tumeziangazia ktk makala zilizopita kwa nadharia zote 5 ikiwemo ya uumbaji maalum ambayo ilizua mjadala mrefu 2)Kama wewe unaamini katika dini na hutaki kupokea concept za sayansi inasemaje na unahisi kama utaingia majaribuni kwa mujibu wa imani yako basi tukutakie safari njema sababu vipande vilivyobaki havikufai na unaweza ukaona kama tunakufuru, sehemu inayokufaa ni part 1, 2 na 3 kuanzia part 4 na kuendelea ni sayansi tupu 3)Nadharia itakayozungumziwa hapa kati ya zile tano tulizojifunza ni nadharia ya "biochemical evolution" tu 4)Katika sehemu ya 4 na kuendelea tutakuwa tukirejea nadharia ya "organic evolution" 5)Mfumo nitakaotumia hapa ni ule Wa rejea(mbele nyuma Kati mbele nk) Naitwa Archimedes Justin

Haya twende kazi,...... Kama tungefanikiwa kuwa na tekinolojia ya kusafiri kurudi nyuma katika muda (time travel) basi Kama tungeamua kurudi nyuma miaka billion 4.5 tukio ambalo tungeliona ni tukio la kuzaliwa kwa sayari yetu pendwa "Dunia" muda huo Wa miaka billion 4.5 tangu kuzaliwa kwa dunia mpaka kufikia sasa umegawanywa katika vipindi vikuu 4 kwa mujibu Wa tawi la geografia liitwalo "geochronology" hili ni tawi maalum la jografia linaloangazia "zama"/era mbali mbali katika dunia kulingana na vipimo vya miamba ya dunia Sasa vipindi hivyo vikuu vinne ni 1)hadean era, 2)Archean era, 3)Proterozoic era na 4)Phanerozoic era Tukianza na kipindi kimoja kimoja,

1/HADEAN ERA hiki ni kipindi ambacho kinachukua muda Kati ya 4.54 billion mpaka 4000 million iliyopita ambacho dunia ilikuwa ni kama tanuru joto la kufa mtu Katika baadhi ya vitabu na machapisho unaweza kuta umeandikiwa Kama ifuatavyo(4540-4000) Mya hiyo isikupe shida mya ni kifupisho cha "million years ago" Kwahiyo itakuwa inamanisha "range" Kati ya miaka million 4540 mpaka 4000 million years ago Sasa mwanzoni mwa kipindi hiki kulitokea mlipuko Kati kati ya wingu zito lenye gas ya hydrogen kwa wingi , huku helium ikifatia na elements zingine zingine kitaalam linaitwa "solar nebulae" Mlipuko huo ulitokeaje?

Kumbuka katika fizikia tunasema hakuna kitu chochote ambacho hakipo kwenye hali ya mwendo hivyo kila kitu kipo kwenye mwendo na hata hizo ges zilikuwa kwenye mwendo zikigongana gongana sasa migongano double double ilipelekea kuongezeka kwa nishati ya ki kinetic na hivyo kufanya kasi ya migongano iongezeke zaidi Kadri muda ulivyozidi kusonga na mwishoe ikafikia kipindi zile punje za hydrogen zilipokuwa zikigongana zikawa zinajikuta zikiungana(fusion) sasa muunganiko huo huwa ni Wa kikemikali ambao hupelekea izaliwe nishati ya joto na mwanga (nuclear fusion reaction) na hydrogen zilipokuwa zikiungana basi zilikuwa zikiunda ges ya helium sasa kilichotokea ni kwamba gesi nyingi zaidi za hydrogen zilikuwa zikivutikia kuingia katika kiini na hivyo kufanya reaction/mpambano uzidi kukolea kadri muda ulivyoenda na kufanya kiini kipanuke zaidi huku joto likiendelea kuongezeka

Sasa tunajua maada ikipata joto hutanuka sio? Na maada yenye uzito Mdogo mfano gesi husogea mbali zaidi kadri joto linavyoongezeka sio? Sasa katika lile wingu kukatokea mpasuko Wa ovyo ovyo sababu ya ongezeko la joto na kupelekea zile malighafi zenye uzito Mdogo kukimbia mbali zaidi na zile zenye uzito Mkubwa kukimbia umbali Mdogo

Lakini tunakubalina kuwa kadri maada inavyokuwa mbali na chanzo cha joto ndivyo inavyozidi kupoa sio? Basi hicho ndo kilichopelekea zile gesi zilizokimbia mbali kupoa na kuanza kuunda vitufe vidogo vidogo ambavyo vilijiunia kani uvutano "surface gravity" (hii niliielezea kqtika makala yenye kichwa kiitwacho "chanzo cha gravity ya dunia") sasa surface gravity ya vigimba hivyo zikapelekea vivute malighafi mbali mbali na kuzidi kuongezeka ukubwa mpaka kuunda sayari na ndio maana unaweza kujiuliza kwanini Jupiter, Saturn, Uranus, na Neptune ni sayari zilizoundwa kwa gesi? Jibu ndo hilo hapo juu rudia maelezo Sasa kwa kesi ya Pluto kule kwenye Ukanda wake "kuiper belt" baridi ni Kali Sana kiasi kwanza zile gas zinapoa na kubadilika kutoka gesi kwenda kimiminika na kupitiliza mpaka kuwa solid na ndio maana Pluto, Charon, makemake na vigimba vingine vyote vilivyoko katika ukanda huo ambavyo tunaviita comets ni solid

Kwa kifupi kuanzia sayari ya Jupiter mpaka Neptune tunaziita outer planets Sasa turudi huku ndani kuanzia mercury mpaka asteroid belt Ukiangalia sayari ya mercury mpak mars zote ni solid na hata asteroids zote ni solid hii ni kwasababu kipindi kile wingu(solar nebulae) inasambaratika sababu ya joto Kali zile malighafi ambazo ni nzito nzito zilishindwa kukimbia umbali mrefu hivyo zikakwamia ukanda huo nazo zikaanaza kufanya mchakato kama ambao nimeuelezea katika "outer planets" uliozipelekea ziongezeke ukubwa na uzito na hivyo kuunda sayari Kwahiyo Ku summarize maelezo yote hayo ni kwamba sayari ziliundwa kwa mchakato ujulikanao kama migongano (collision) Mwaka 2003 wanajimu Wa nchini marekani walienda angani kufanya jaribio la hiyo nadharia kwa kutumia chumvi ambayo waliiweka kwenye mfuko mweupe/transparent mpana na kwakuwa katika space gravity ya dunia ni sifuri vilevipande vya chumvi vikawa vinajiundia gravity zao na kuanza kugongana na kuunda vimanundu manundu huo ulikuwa ni ushahidi tosha kuwa sayari ziliundwa kwa kutumia mchakato huo Sasa tukija katika upande Wa dunia tunaona kuwa dunia yetu Ina satellite ya asili/mwezi je ulitokeaje?

Tukibaki katika "collision theory" inasadikika kuwa gimba lenye ukubwa Wa kama sayari ya mars lililopewa jina la "theia" liligongana na dunia yetu at a certain angle na hivyo kupunguza ukubwa wake kwa kuacha malighafi zake nyingi hapa duniani na vumbi kubwa la moto lilitimuka angani na kupelekea lipoe polepole huku likijikusanya na kuunda kagimba kadogo ambako ndo mwezi tunaouona Katika kulithibitisha hilo mnamo mwaka 1972 wanajimu Wa nchini marekani walitua mwezini na kuchukua kipande cha mwamba na kurudi nacho duniani na wataalam Wa miamba walipokipima waligundua kina madini Kama haya ya kwenye uso Wa dunia (crust) hivyo kwa jaribio hilo ilikuwa ni ushahidi tosha

Sasa katika kipindi hicho gravity ya dunia iliweza kushikiria gas mbali mbali angani mam vile hydrogen, nitrogen, carbon dioxide, noble gases na water vapour isipokuwa oxygen yenyewe ilikuwa kwa kiwango kidogo sana ila ilikuja kuundwa baadae Katika kipindi hiki cha "hadean" Hapakuwa na uhai wala dalili za uwepo Wa kiumbe hai Dunia ilikuwa ni uji Wa moto

Joto lilikuwa Kali kupita maelezo Na ndio maana kipindi hichi kimepewa jina la "hadean" lilitokana na hellish ambalo ni kivumishi cha nomino hell sasa maana ya hell ni kama kuzimu/jehanam/mahari penye joto Kali nk 2)ARCHEAN ERA tutaendelea sehemu ya 5 panapo majaaliwa

JE BINADAMU ALITOKEA WAPI.

SEHEMU YA 5

Katika sehemu ya 4 tuliona zama iitwayo "hadean" Kama bado hujaipata peruzi profile yangu,... Sasa Leo tutaangalia zama ya Pili iitwayo Archean era

2)ARCHEAN ERA

Hii ni zama ambayo inakadiliwa kuwa Kati ya kipindi cha miaka 4000 million mpaka 2500 million BC NOTE:kuna changamoto niliiopokea jana kuhusu namna ya kuandika miaka kwanini inaanzia namba kubwa inafatia ndogo? Mfano ni hapo (4000-2500million years) BC hii ni kwasababu muda Wa dunia umegawanya katika sehemu kuu mbili

1)muda uliokuwepogo kabla yesu hajazaliwa (before Christ BC) 2) muda ulioanzia yesu alipozaliwa mpaka sasa na kuendelea(anno domin AD/baada ya yesu kuzaliwa) Sasa ili uelewe ngoja nikupe mfano mwepesi Fikiria labda umbali Wa kutoka ubungo hadi mbagala ni 12 km Lakini buguruni ndo Kati Kati na umbali kutoka ubungo hadi buguruni ni kilometa 6 Sasa kwakuwa buguruni ni Kati Kati basi tuseme umbali Wa buguruni ni Kama buguruni ni km 0 Kwahiyo ubungo to buguruni itakuwa 6 km na buguruni to mbagala itakuwa 6km sio?

Sasa fikiria wewe upo mbagala alafu baby wako anakuja kutoka ubungo maana yake atakuwa Kama anaporomoka kutoka kilometa 6 kuelekea kilometa 0(ubungo) kisha aanze kupandisha tena kilometa mpaka afike mbagala ambapo atatembea kilometa zingine 6 (kutokea buguruni) sio? Sasa kumbuka tabata matumbi ipo Kati Kati ya ubungo na buguruni(3km kutoka upande wowote) Kwahiyo akifika tabata matumbi tutasema ametembea umbali Wa (6-3)km maana kaanzia ubungo(6km kutoka buguruni) kashuka hadi matumbi(3km) Si umeona inavyoleta maana?

Sasa fikiria tunazungumzia muda kwahiyo badala ya kilometa chomeka muda katika vizio vya miaka alafu umbali Wa ubungo mpaka buguruni uwe ndo BC na umbali Wa buguruni mpaka mbagala uwe ndo AD alafu buguruni ndo zama alizozaliwa yesu hivyo inasimama Kama point of reference Natumaini nitakuwa nimekujibu,.... Sasa tuendelee na makala yetu Naitwa Archimedes Justin

Napatikana kwa 0622181966WhatsApp Katika kipindi hiki cha Archean era, dunia ilipoa kwa kiwango kikubwa na kufanya ujiuji katika maeneo yote kuganda na kuunda ardhi kavu "crust" na hivyo kupelekea hata angahewa kupoa na hivyo zile "water vapours" zilianza kubadilika kutoka kwenye gaseous state na kuwa liquid state na hivyo kushuka Kama mvua na kujaza mabonde mabonde makubwa kwa madogo ambayo Leo ndo tunayaita bahari na maziwa Pia kipindi hiki cha Archean ndo kipindi ambacho viumbe hai walianza kuchomoza na viumbe hai hao ni wale "cells" Wa awali au wanaitwa "pre-existing cells" Kama cell theory inavyotuambia katika tawi la baiolojia liitwalo "cytology" Sasa cell ni nini? Cell ni kiini cha chini kabisa cha uhai ambacho ndo chimbuko la uhai Kila kiumbe hai unayemjua wewe hapa duniani ameundwa kwa cell

Inaweza kuwa cell moja au muunganiko Wa cells zaidi ya mbili Kama atakuwa kaundwa kwa cell moja basi kibaiolojia tunamwita "unicellular organism" mfano ni bacteria na Kama ameundwa kwa muunganiko Wa cell zaidi ya moja basi tunamuita "multicellular organism" mfano ndo binadam ambaye tunamuangazia alitokeaje Sasa hizo cells zina sifa gani na zilitokeaje? Cells zinasifa nyingi ingawa sifa kuu za cell ni hizi zifuatazo

1) cell lazima iwe na vinasaba/genetic materials 2)cell lazima iwe inakiminika kilichoundwa ambacho asilimia kubwa ya kimiminika hicho ni maji Kimiminika hichi tunakiita "cytoplasm" 3)cell lazima iwe na uzio wake/cell membrane Sifa zingine ni za ziada na hutofautiana kutoka cell moja hadi nyingine mfano mitochondria, plasma reticulum, vacuole, cell wall, nk Sasa cells hizo za awali zilitokeaje? Namna zivyotokea ni kwa bahati nasibu/Kama zali/probability (Hapa Kama una idea ya quantum physics utaelewa mchezo unaoitwa "quantum probability" ambao niliwahi kuuelezea katika makala iliyokuwa na kichwa kisemacho "je electron ni punje au wimbi?") Sasa katika sehemu ya Pili tulijifunza kuhusu "miller's experiment" iliyofanywa na Stanley miller miaka ya 1950s ambapo alichukua gas za methane, ammonia, hydrogen,na water vapour na kuziweka katika kifaa maalum maabara na kupitisha "electric field" ambapo mwisho Wa siku ziliungana na kuunda compound iitwayo "amino acid" ambayo amino acid ni Kama tofali za kiumbe hai chochote hivyo kwa muktadha huo tunaamini kuwa hata utokeaji Wa cells za kwanza ulitokea katika namna hiyo au kwa mchanganyo Wa namna nyingi nyingi kulingana na "probability"

Chukulia mfano umempa ngedere computer abonyeze bonyeze keyboard obviously atakachokuwa anakiandika kitakuwa ni utumbo sio? Ila kadri anavyobonyeza bonyeza anaweza kujikuta kaandika neno moja lenye maana labda tuseme neno "that" fikiria akaendelea kubonyeza bonyeza anaweza akajikuta kaandika neno "is" na akiendelea kubonyeza zaidi anaweza kujikuta kaandika neno "life" sasa fikiria maneno yote yenye maana yameungana katika mpangilio maalumu kulingana na "probability" basi itasomeka "that is life" unaona tunapata sentesi yenye maana kabisa hivyo hivyo ndivyo ilivyotokea katika mchakato Wa kutokea kwa cells za awali kulikuwa kunatokea "summation of multiple probabilistic events" ambyo ilipelekea kuzaliwe utumbo/vitu vya ovyo ovyo na vitu vya maana kama tulivyoona katika mfano Wa ngedele Sasa nikurudishe juu katika sifa ya kwanza ya cells, tumesema kuwa cells lazima ziwe na vinasaba/genetic materials je genetic materials ni nini?

Katika makala yangu ya "From what is physics to the theory of everything" part 1 niliwahi kuelezea vinasaba ni nini Ila na hapa nitakazia Vinasaba/genetic materials ni materials ambazo zimebeba sifa zote za kiumbe hai mfano hiyo rangi yako ya mwili imetokana na vinasaba ulivyonavyo Sasa kama tutasafiri na kuingia mdani ya cell(fikiria cell ni mam nyumba) basi lazima kwanza tuvuke uzio(cell membrane) tukishavuka uzio tutakutana na Maji Maji(cytoplasm) na katika eneo hilo la Maji Maji tutakutana na vitu vingi sana kama vile vacuole, chloroplast mitochondrion, plasma reticulum, cell body nk kulingana na cell tulioingia Sasa kama utakuta katika eneo hilo kuna genetic materials zinaambaa ambaa tu bila mpangilo basi cell hiyo tunaiita "prokaryotic cell" au kiumbe chenye cell hiyo tutakiita "prokaryote" mfano ni Bactria

Ila kama utakuta kuna kiini maalumu chenye uzio ndani ya hiyo cytoplasm na ndani ya kiini hicho ndo kuna genetic materials basi cell hiyo tutaiita "eukaryotic cell" na kiumbe chenye cell hiyo tutakiita "eukaryote" mfano ni binadam ambaye ndo tunamuangazia alitokeaje Sasa ebu tuziangazie sifa za genetic materials kimuundo

Kwamba tambua kuwa kuna aina mbili za genetic materials 1)DNA(deoxyribonucleic acid) nazani kwa wale mliosingiziwa mtoto mshakutana na kauli "twende tukapime DNA" sio? 2) RNA(ribonucleic acid) Sasa aina zote hizo mbili hufana kwa asilimia kubwa zote zina sifa kuu tatu 1)zina carbohydrate iitwayo "ribose sugar" 2)zina "phosphate group" 3)zina nitrogenous bases Ila utofauti wao ni kwamba DNA inaumbo ina mistari miwili mirefu, RNA Ina mstari mmoja mrefu DNA ina upungufu Wa oxygen 1 katika ribose sugar yake wakati RNA Ana ukamilifu Wa oxygen zote 5 DNA Ina compound iitwayo "thymine" katika nitrogenous bases zake wakati RNA Ina compound iitwayo Uracil badala ya thymine katika nitrogenous bases zake

Mara nyingi RNA hutengenezwa na DNA katika mchakato ujulikanao kama "DNA transcription" Sasa tuanze na moja moja kuichambua DNA Hii ni material ambayo inkuwa na umbo kama ngazi ambayo imesokotwa na kuunda nane nane zinazojirudia kulingana na urefu wake, kila nane tunaiita "DNA molecule" ambayo inakuwa na phosphate group, ribose sugar na nitrogenous base Sasa inakuwa ndefu kiasi cha kuunda burungutu kama kamba ya kufumia vitambaa sasa burungutu hilo ndo tunaliita "chromosome" Sasa fikiria unakunjulua hilo burungutu basi utakuwa na kamba ndefu sio? Sasa fikria unakata kata kamba katika vipande vipande kwa kuangalia nane nane kadhaa basi vipande hivyo ndo tunaviita "gene"ambavyo ndo hubeba sifa mbali mbali za kiumbe hai na kila kipande huwa na sifa yake ambayo hukaa katika namna ya ukinzani mfano ufupi na urefu, unene na wembamba, akili na ukilaza, weupe na weusi, nk ambapo katika kipengele za uzalianaji kwa viumbe ambao hujamiana lazima kutokee segregation katika genital epithelial cells(cells za awali za uzazi) ili kusudi sifa moja Kati ya hizo mbili ndo iende kwenye yai au sperm mchakato huo kwa jina lingine huitwa "meiosis" Sasa tukirudi pale juu niligusia nitrogenous bases ambazo pia zinaonesha utofauti Kati ya DNA na RNA Sasa nitrogenous bases ni nini?

Nitrogenous bases ni materials complex ambazo zimeundwa kwa muunganiko wa element nyingi nyingi tofauti ila kuu ni nitrogen Nitrogenous bases hizo ni Thymine, uracil,adenine, cytosine, na guanine, Sasa base hizi hushikana kwa kuendana kama ifuatavyo kwa upande Wa DNA T-A C-G hapo inaweza ikaendelea kulingana kwa mchanganyo kutokana na urefu Wa DNA structure kama ifuatavyo C-G T-A G-C A-T kikubwa tu T i match na A wakati C Ina match na G Sasa kwa upande Wa RNA utofauti Wa hizo nitrogenous bases upo kwenye Thymine Badala ya thymine kunakuwa na uracil ambayo ita match na Adenine na bases zingine zilizobaki zinaendelea kama kawaida mfano U-A C-G A-U G-C hivyo hivyo na kuendelea Sasa kumbuka nimekuambia Mara nyingi RNA inaundwa na DNA katika mchakato uitwao "DNA transcription" sasa hapo tutajiuliza je uracil inatoka wapi? Wakati katika components za DNA hatuioni? Stay connected to part 6 NOTE kuna mmoja naona alinipa ofa ya bando la internet napenda kumshukuru sana pia kama ukiguswa namba iko hapo juu Na kwa wale walioomba nifungue kundi la WhatsApp nipende kuwaomba radhi sitafanya hivyo sababu muda Wa kuratibu group sina Kwa huduma za vitabu soft copy nicheki kwenye number 0622181966whatsapp huduma ya vitabu ni bure narudia tena huduma ya vitabu ni bure kuna vitabu mbali mbali kama vile sayansi, dini,mapenzi, uchumi, saikolojia na tunaweza kuvijadili kwa pamoja endapo kunasehemu utapata utata na ndio dhumuni la hiyo namba ya WhatsApp kuwepo hapo nk Knowledge is unending adventure never stop learning

Posted on August 14, 2021 | Categories:

Thursday, August 12, 2021

FAHAMU NINI MAANA YA INFARED RADIATION

INFRARED RADIATION

Nimeona Leo nielezee Kuhusu Infrared Radiation zitakazokuwa zinatazamwa na Kifaa kimoja cha anga kinachoitwa James Webb Space Telescope (JWST)

Nitaanza kushusha Uzi wa Series wa Hicho chuma ambacho kitapaishwa mwisho mwa mwezi wa 11, Chuma kilichochukua thamani ya Dola za kimarekani bilioni 10 (kwa bajeti ya mradi iliyowasilishwa 2016) JWST itakuwa na uwezo wa kung'amua mawimbi ya Infrared. Yenyewe sio kama Hubble Space telescope ambayo ilikuwa inaweza kung'amua (vizuri) mawimbi ya Ultraviolet (UV) na kipande kidogo cha kuonekana (Visible light).

Hiyo itakuwa ni siku nyingine. Sisi kwa leo tuingie kwenye mionzi na tuangalie mionzi ya Infrared. Una ubavu wa kusoma.!? Kama una uwezo wa kusoma, soma, Kama hauna uwezo, tafuta uwezo, Ili mradi usome Nini maana ya INFRARED radiation.!?

Unajua kuna mionzi ya umeme na sumaku (Electromagnetic radiation). Alafu vile inavyokuwa inasafiri inasafiri kama mawimbi (waves) yaani inafanya propergation ya Juu-chini, chini-juu, kulia-kushoto, kushoto-kulia. Tuseme inanyumbulika kama NYOKA,

hapo inakuwa inafyatula kwa Speed ya karibu kilomita laki tatu kwa sekunde. Mionzi ikiwa inasafiri na kuunda mawimbi huwa ni Electromagnetic waves, Lakini zote hizo ni radiation zanazosafiri. Kwa hiyo usije tena kuchanganya kati ya Radiation na waves. Hapo tuko sawa.!?

Sasa wakati mawimbi yanaundwa kunakuwa na kupanda juu (mlima/Crest) na kushuka chini (bonde/trough) Kule kupanda juu au kushuka huwa na umbali wake (umbal/urefu wa mlima au bonde) Urefu huo huitwa "Amplitude". Fatilia waves utaelewa. Kwenye mawimbi kuna "wimbi kamili" Yaani hapa "urefu wa wimbi moja" Hii huitwa "Wavelength"

Tuelewane hapa urefu wa kupanda juu sio urefu wa wimbi (kifizikia) Urefu wa kupanda juu (kwa mfano mawimbi ya maji) unaitwa amplitude, Urefu wa wimbi (Wavelength) unapatikana kutoka "kilele cha mlima mmoja hadi kilele cha mlima mwingine" Au shimo la bonde moja mpaka shimo la bonde lingine. Au point mbili ambazo ukiungunisha mlima mmoja na bonde moja unaunda mduara. (Dah haya masomo mengine mpaka tungekuwa live tunachora, ila utakuwa umeelewa, angalia picha hapo chini.) Sasa ulishajua urefu wa wimbi moja (Wavelength) basi tutaenda sawa,

Mawimbi yakiwa yanasafiri, huwa yanapungua nguvu (Frequency/Energy) Hapa kwenye kupungua Frequency huwa yanabadilika urefu wa wimbi. Tuchukulie mfano, baharini unaogelea, Mawimbi yakiwa yanakuja kwa "Speed" ya haraka, Yani yanakupiga kwa haraka sana bila kukupa mda wa kupumzika, hayo ndo yanakuwa yana NGUVU, Yaani yale mawimbi ambayo halijaisha hili limekuja lingine, haujapumua limekuja lingine, hayo yanakuwa yanakuja karibu-karibu, Ndio huwa tunasema yana nguvu. Sijui kama unaelewa,

Lakini yale ambayo yanapiga, unasubiri baada ya sekunde 5 ndio linakuja lingine, linaipita, unatulia baadaye linakuja lingine, Hay huwa HAYANA NGUVU. Kwa hiyo yale ambayo huwa "kutoka mlima mmoja hadi mwingine ni pafupi", tunasema yana "short wavelength" (urefu wa wimbi mfupi) hayo tunasema yana Frequency (energy/nguvu) kubwa. Yale ambayo huwa, "kutoka mlima mmoja kwenda mwingine" ni parefu tunasema yana "long Wavelength" (urefu wa wimbi mrefu) hayo huwa yana Frequency (energy/nguvu) ndogo. Hayeee, hapo vipi.!?

Nitawajazia picha picha hapo chini, fatisha na maelezo lazima utaelewa tu, Naamini siwezi kukupoteza. Umechoka.!? Tumalizie... Mawimbi ya Electromagnetic yakiwa yanatembea huwa yanapoteza nguvu kwa umbali ambao huwa yanaenda, Hivyo huanza kuongezeka Wavelength. Mfano mawimbi ya Ultraviolet huwa na Wavelength ndogo kuliko Infrared hivyo UV ina Frequency kubwa kuliko Infrared. Pia baada ya Infrared huwa inafata Microwave, na mwishoni mawimbi ambayo hayana nguvu sana Huwa ni Radio wave. Radio wave tumeona kwenye post ya mtu mmoja humu simkumbuki, inaweza kuathirika na static electricity ya nguo baada ya ku-pasi (haina nguvu)

,

Sasa naona umebobea kwenye mionzi na mawimbi, Sasa twende Infrared yetu. .......... Infrared ni kipengele cha mawimbi ya Umeme na sumaku (Electromagnetic waves) ambacho mawimbi yake huwa na ukubwa kuanzia nanomita 750 hadi milimita 1 (750nm - 1mm) Hiki ni kiasi kidogo sana, hata hivyo hii mionzi haionekani kwa macho Mionzi inayoonekana kwa macho (visible light/radiation) ina urefu wa mawimbi kunazia 340nm hadi 750nm Hivyo inapoishia tu Visible light (rangi nyekundu) ndipo huanzia Infrared. Mda mwingine utaona wanakwambia Infrared inaanzia 780nm, kile kipande cha 30nm kutoka Visible light hadi Infrared huitwa "Red infrared" ila sisi wataalamu wa Spectrophotometry tukiite tu chote ni Infrared. Kuna Red Infrared, kipande kinachokaribia red light band kwenye Visible light, mda mwingine huitwa "Near Infrared" Kuna Mid Infrared hii huanzia kwenye 780 yenyewe hadi kitu kama 850 hivi, (Sina uhakika hapa inabidi nirudi kupiga pindi, haya mambo ni mengi hapa nawapa kwa kurashia-rashia tu, lakini nina imani mnakuwa wabobezi hapo.)

Hiyo ndio Infrared kwa kiasi nachoweza kuwafundisha kwa sasa, Kuanzia 750nm, tufanye 780nm ambayo wao wanapendelea hadi 1mm. Huo ni ukubwa wa Wavelength.

Ni sawa na wanafunzi wa sekondari kutengwa kuitwa hawa ni from one hawa ni form 2, 3, 4 nk ni ile uwezo wa mambo wanayoelewa shuleni na mda waliosoma, Ila wote ni wanafunzi wa sekondari. Hata Mionzi, yote ni mionzi, inatengwa kwa sifa mbalimbali, Ila sifa moja kuu ya kutenganisha mionzi hiyo ni UREFU wa mawimbi yake (Wavelength) Hapo itakuja mionzi mbalimbali kama Gamma, x-ray, Ultraviolet, Infrared, Microwave, Radio, Betta na mingine. Ila yote ni Mionzi (Radiation)

Maelezo na Cekams Cekam

Posted on August 12, 2021 | Categories:

FAHAMU MAANA YA LIGHT YEARS AU KIPIMO CHA MIAKA YA MWANGA

FAHAMU MAANA YA KIPIMO CHA MIAKA YA MWANGA

Iwe ni mwanga wa laser, tochi, umeme, kibatari au mshumaa, Mwanga ni mwanga. By thay way, tukitumia makadirio.... Hipo hivi.

Kwa sekunde mwanga unasafiri kilomita laki 3. (300,000km/s) Tuanze conversation... Dakika moja ina sekunde 60... Saa moja lina dakika 60... Siku moja ina saa 24... Wiki moja ina siku 7 tutumie mwezi wenye siku 30, Kwa hiyo mwezi mmoja una siku 30... Mwaka una miezi 12... Kwa hiyo tukitaka kufahamu mwaka una sekunde ngapi tutafanya kuzidisha kwa kumaainisha mmoja anamzaa mwenzake mpaka mwaka mzima ukamilike Itakuwa sekunde kwenda saa, kwenda siku, kwenda mwezi kwenda mwaka. Tutaanzia superstructure (mwaka) hadi substracture (sekunde) Kama hivi....

1×12×30×24×60×60= =31,104,000 Nilimaanisha, "mwaka 1 una miezi 12, kila mwezi una siku 30, kila siku ina saa 24, kila saa lina dakika 60, kila dakika ina sekunde 60. Jumla= 31,104,000 sekunde kwa mwaka mzima. Tuko sawa!?? Sasa twende umbali ambao mwang unausafiri kwa mwaka mzima, Tunajua Speed ya mwanga ni 300,000km/sec Tuna sec 31,104,000

So, 300,000 × 31,104,000= =9,331,200,000,000 9,331,200,000,000 Hii ni Trilioni 9, bilioniii 331, na milioni 200, Mmmh na wew isome. Kwa hiyo mwanga unatembea kilomita 9,331,200,000,000 kwa mwaka. Huoni hii inatusumbua kuisoma, sasa bora tukasema "urefu wa mwaka wa mwanga" kuliko kusema hiyo namba kubwa mno. Kwa hiyo ukisikia kuna sayari inasadikika kuwa viumbe kama binadamu wanaweza kuishi, inaitwa Kepler 10b Ipo umbali wa... "Bilioni 12 miaka ya mwanga"

Ujue iko "kilomita bilioni 12 mara hiyo namba" Hahahahhaah, tukisema ni mbali nafikiri vipi sijui, Yani ni mbali haswa, mbali. 12 bilions light years iko hivi... 12,000,000,000× 9,331,200,000,000 =111,974,400,000,000,000,000,000km Duh, tutumie standard notation =1.119744×10²³km Hiyo ndo 12 bilion light years. (Umbali ambao, kama unasafiri katika speed ya mwanga {300,000Km/s} bila kusimama (non-stop), itakuchukua miaka bilioni 12 njiani, hahahahahha ) Unaona urahisi wanasayansi waliotumia ili namba zisikuchanganye. Kumbuka Observable Universe ni 75 bilions light years.

Maelezo na cekams cekam

Posted on August 12, 2021 | Categories:

JUA LINAZUNGUKA ? LINAZUNGUKAJE ?

HIVI JUA LINAZUNGUKA??

Jua ni nyota iliyo karibu na sisi (Dunia)

Ni nyota ambayo inazungukwa na sayari takriban 8, ukiondoka Pluto ambayo kila mara inapoteza sifa zake za kuwa sayari. Muunganiko wa sayari, miezi, vimondo, asteroidi na mawe-mawe na gesi chafu za angani zinazozunguka Jua huunda mfumo wa Jua (solar system) Dunia ni sayari ya 3 ukitokea kwenye jua katika mpangilio wa sayari zinazo zunguka Jua Jua ndilo linalotoa nguvu ya nishati, na mwanga kwa aslimia 99% kwenye mfumo wake, Jua huwa na nguvu ya mvutano (Gravity) kubwa sana, kuweza kushika au kuvuta vitu vyote kwenye mfumo wake ili bila kupotea, vibaki vikilizunguka kila kimoja kwa njia yake na mwendokasi wake (speed) Jua ni miongoni mwa Nyota nyingine nyingi zilizo katika kikundi cha nyota (galaksi) kinachoitwa Milkway (Milkway galaxy) ▪️Je, Jua linazunguka? ▪️Linazunguka nini? ▪️Linazungukaje?

By the way, Jua linaaaminika kuzunguka kwenye galaxy yake, Mzunguko mmoja wa Jua huchukua miaka milioni 200 na.... Kila nyota kwenye Galaxies ipo katika motion kuzunguka kwenye galaxy. Uliwahi kujibiwa swali la kwanini Galaxies zinaunda spiral pattern?? Kwa sababu kila kitu kinazunguka.

Kama sayari zinavyozunguka jua, na Nyota zinazunguka blackhole. Moja ya blackhole yenye nguvu ambayo nyota zinazunguka inaitwa Sagittarius A, hii ni Blackhole katikati ya Milkway galaxy. Galaxies zinaonekana kama CD (Compact Disk) Disk inakuwa na band mbali mbali, ukichukulia CD ya movies tuseme zile band ndo rangi, Basi pale katikati ndo kuna hilo Blackhole, Kumaanisha nyota zinazunguka blackhole,

Chukua ile CD weka peni katikati zungusha, au vile CD inakuwa inazunguka kwenye DVD (hujawahi kuona) Basi vile feni linakuwa linazunguka, Unapata picha, eeh!!

Kuna nadharia ya kwamba nyota au pamoja na sayari na vitu vyote vinatembea kwenye 3 Dimensions. Yaani katika njia ya kuzunguka na kuhama. Kuna ile kwamba jua linahama (move) pamoja na galaxy yake. Mfano huu utakuwa unaongelea "motion in straight line" Kwamba kama Universe ina-expand basi galaxy zinaama in straight line kuelekea mbali Tutumie CD

Sasa weka CD kama 5 kwenye meza kumaanisha Galaxies, ziweke umbali wa karibu-karibu Ili kusema universe ina-expand basi zile CD zivute kuelekea mbalimbali ziachane. Unaona, Galaxies zimeenda kwenye straight line, ( lectlinear motion). Na hapo utona kuwa hakuna kuzunguka. Lakink tunavyosema kuzunguka na kuhama kwa pamoja kuna motion mbili, wakati CD inazunguka na bado hapohapo inatembea. Sasa kuelewa hii, chukua CD irushe angani ukiwa unaizungusha, huo mwendo ndo mwendo wa Galaxies kwenye space Twende kwenye ku-expand, Chukua CD 5 zote mkono mmoja, Zirushe kwa kuzizungusha,

Angalia matokeo huko mbele kila moja itachuka njia yake na kuachana, (Expansion) Lakin zilikuwa na motion 2 1: zinajizungusha 2: zinatembea zikiachana Hapo kwa kutumia galaxy, jua litakuwa linamizunguko miwili, ▪️Kuzunguka blackhole (revolution) na ▪️Kutembea na galaxy (universe expansion) Hii ni 3D, x,, y,, na z,, Basi Dunia itakuwa na motion 3, ▪️Kujizungusha ▪️Kuzunguka Jua na ▪️Kuondoka na jua kwa vile jua linaondoka na galaxy Kwa hiyo kila kitu ili kiweze kufanya movement kwa njia ya kuhama lazima kijizungushe. (Kwenye space) Kama hivi...

Chukua mpira, ukiwa umeutuliza sehemu, uuzungushe (rotation) Hautatulia lazima utaanza kutembea, Tena sio kutembea tu, ni kwenye "Curved (circular) path" Gari likiwa kwenye speed likitaka kukunja kona kwa speed lazima liwe kama linazunguka kwenye rotation, Hii inawezekana kusema jua lina rotation, japo ni kubwa hatuwezi kuligundua haraka, na kwa kuwa wanasayansi hawajajikita kufatalia jua ndo maana hawajataka kusema, Na mimi leo ninasema "Jua lina rotation, nipeni vifaa niwape Proof"" Rudisha mawazo kwenye CD ukiirusha kama tulivyosema utaona kama inakunja kona kukurudia, Hivyo ndivyo galaxy zilivyo... Hapo chini nawapa picha ya Milkway galaxy, uweze kuona "Disk bands" Jua linazunguka centre ya Milkway galaxy. Naongeza "Jua lina rotation"

Maelezo na Cekams Cekam

Posted on August 12, 2021 | Categories:

UKUBWA WA ULIMWENGU NA YALIYOMO

Mars pengine ndio sayari maarufu kuliko zote kwenye solar system pamoja na kwamba iko mbali lakini inatoa viashiria vya uwepo wa maisha hapo zamani miaka mabilioni iliyopita.

Wanasayansi kutokakna na viashiria nilivyotaja huko nyuma wanajaribu kuangalia ni kwanini maisha kwenye Mars hayapo lakini yakawepo kwenye dunia yetu na je kilichosababisha nini maisha yakatoweka.Hii itatupa picha na sisi dunia yetu hapo baadae pengine maisha hayatakuwepo. Mariner 4 ya Marekani ilikuwa ndio probe ya kwanza kutembelea Mars.Hii ilikuwa ni mission ya kuivinjari tu Mars kwa maana rahisi ni kuwa ilikwenda tu na kuchukua picha za sayari hiyo. Picha hizi ndio zilikuwa picha za kwanza kabisa kupigwa karibu .Hizo picha ziliwakatisha tamaa sana wanasayansi kwa kugundua hakuna mifereji kama ya kupitisha maji bali waliona maelfu ya craters kama ilivyo kwenye mwezi.

Miaka minne baade baada ya binadamu wa kwanza kukanyaga ardhi ya mwezi , Mariner 6 na 7 zilipiga picha zingine. Zilifanana na zile zilizopigwa na Mariner 4. Tena wanasayansi walikata tamaa kwa kugundua sayari ni sayari mfu kuliko walivyodhania. Mariner 9 mwaka 1971-1972 iliweka kwenye orbit kuizunguka Mars ili kuchukua picha za ardhi yote ya Mars kwa ujumla wake.Ingawaje muda inapiga hizo picha Mars ilifunikwa na kimbunga cha vumbi maana yake ni kwamba sehemu ya ardhi yake haikuonekana vizuri.Mwishoni mwa mission hiyo vilele vinne vilionekana juu ya mawingu ya vumbi hilo.Hivyo vilele vilikuja kuonekana ni volcano.Hii ilikuwa ni dalili njema kwao ya

kuonyesha kuwa kwenye Mars kuna maisha ya ki jiolojia ya kuweza kufanya utafiti. Volcano kubwa kuonekana na chombo cha Mariner 9 pia ndio volcano kubwa kuliko zote katika mfumo wa jua.Inaitwa Olympus Mons na ni ndefu kwenda juu mara tatu ya mlima mrefu kuliko yote duniani wa Everest ina urefu wa kilometa 27 kwenda juu nilishaelezea huko nyuma. Pia kulionekana uwanda wa lava uliosababishwa na volcano hizo,Pia kulionekana magema na mifereji ambapo hapo zama za kale maji yalipita.Uwepo wa volcano inaonyesha kuwa hapo zama za kale Mars ilikuwa na kiini cha moto kama ilivyo dunia yetu. Lakini swali linakuja je sayari hiyo bado ina kile kiini cha moto? Je volcano hiyo inaweza kulipuka? Wamarekani mwaka 1975, walirusha vyombo vinaitwa Viking probes.Hizi probe ndio zilishuka kwenye sayari hiyo kwa ajili ya kupiga picha ardhi ya Mars na kupima kama chini ya kiini chake kuna mtetemeko wowote kuonyesha kwamba kuna uwezekano wowote wa mlipuko wa volcano.Viking 1 ilipiga picha za kwanza nzuri kuonyesha kuwa Mars ni sayari jangwa yenye miamba myekundu na anga lake likiwa la rangi ya pink.

Picha chini kwa juu inaonyesha volcano kubwa kuliko zote kwenye solar system inaitwa Olympus Mons hiyo inaonekana kama ndogo lakini ukweli ni kwamba ina kimo cha kilomita 27 na safu ya mlima kwa umbali wa kilomita 600 kwa upana.Picha hii imepigwa na chombo cha Hope kilichorushwa na umoja wa falme za kiarabu UAE tarehe 26 february 2021 na kutua sayari ya Mars

Maelezo na Daudi Mbaga

Posted on August 12, 2021 | Categories:

FAHAMU KUHUSU CHOMBO KIPYA CHA STARLINER

Chombo cha starliner kuelekea kwenye kituo cha anga cha kimataifa ISS leo, ni safari yake pili ya majaribio (orbital flight test-2). Chombo hiki kimetengenezwa na Boeing kwa ushirikiano na NASA. Na kitarushwa na rocket kutoka kampuni ya ULA, naizungumzia Atlas V N22 rocket. Kabla hatujaenda mbali Boeing's starliner capsule inashikilia record - ya kwamba ndio capsule ya kwanza ya mmarekani kutua kwenye ardhi (2019).

Kumbuka hizi capsule nyingine zikiwa zinarudisha watu duniani huwa zinatua kwenye bahari, lakini hii starliner imedizainiwa kutua kwenye ardhi - landing system yake itahusisha ma-parachute kama kawa lakini pia airbag Starliner ina seat saba za kukaa na sehemu ya kutosha ya mizigo, na ndani ndio kama hivyo unaweza kusema studio ya next level music 😁 note: kwa safari ya leo chombo hakitabeba mtu. Hii starliner buana itafanya docking automatically (kuungana na ISS) na si docking tu mpaka rendezvous ni autonomous.

Maelezo na Ipuli

Posted on August 12, 2021 | Categories:

FAHAMU INTERNET INAPATIKANAJE KWENYE ISS

INTERNET KWENYE ISS

Umewahi kufanya screen mirroring kwenye laptop na laptop au Tv, au simu na simu - yaani kufanya kinachonekana kwenye screen hii ndio kionekane kwenye screen yingine? Kwa yeyote aliyewahi kufanya hivyo hata kwa simu basi simu kichwani kwake itamjia kumbukumbu ya Airplay - kama ni mdau wa Apple. Au chrome cast, team viewer na nk - kama ni mdau wa Android. Sasa hii screen mirroring inahusikaje hapa na wakati sisu tunataka kujua kuhusu internet kwenye ISS..?

Well, internet kwenye ISS sio direct kama kwenye smartphone au laptop yako - namaanisha laptops na tablet ndani ya ISS zimefanyiwa screen mirroring na laptops nyingine huku duniani.

Hivyo basi jamaa kule ndani ya ISS anaposhika laptop au tablet na kuingia mtandaoni labda Facebook, akawa anapitia-pitia post za ipuli boi na labda labda akaipenda post yangu kuhusu na aka-comment "safi mdogo wangu"😁 Kiuhalisia ile tablet au laptop aliyoshika sio ambayo imeingia FB na kutuma hiyo comment kwenye servers za Facebook. Au kwa lugha rahisi niseme sio ambayo yenye bando (japo sio sahihi sana kusema hivi). Itakayotuma hiyo comment ni laptop iliyoko huku duniani - ambayo kimsingi imefanyiwa screen mirroring na ile ya kwenye ISS.

Kwahiyo mchakato utakuwa hivi - comment ya jamaa itaenda kwenye LAN sever (Local access network) ndani ya ISS, kisha itapelekwa kwenye Ku band antenna - ambayo iko upande wa unaongaliana na space.

Hii antenna itaisafirisha hiyo comment mpaka kwenye TDRSS (tracking and data relay satellite system) - ambazo zipo kilomita 35000+ huko. Sasa hizi satellites ndio hutuma signals huku duniani sasa - comment ndio inakuja hivyo.

Signals hupokelewa na ma-dish yaliopo pale mjini new Mexico. Baada ya kupokelewa comment ya jamaa itaingia kwenye NISN network na kuelekea kwenye mission control center - hapa mission control center sasa ndio kuna laptops zimefanyiwa mirroring na za kwenye ISS. Ikifika kwenye laptop iliyofanyiwa screen mirroring - mchakato mmoja unakuwa umeisha, unaanza wa pili. Laptop ya hapo control center ndio huingia internet kama laptop nyingine au kama simu yako tu.

Namaanisha kupitia network provider (mfano. Tigo) kuelekea kwenye servers za Facebook. Na jibu linapotoka kwenye server za Facebook hupitia mlolongo huo huo - kinyume chake kurudi kwenye ISS. Computers za pale mission control center na computers zote za NASA zipo restricted na idara ya Usalama ya IT, na website zisizohusiana na kazi zimeblokiwa hivyo wanaanga hawaulizani 'una-download au unaangaliaGa humo humo'😁

Maelezo na Ipuli

Posted on August 12, 2021 | Categories:

NEWTON GRAVITATION THEORY NA EINSTEIN GENERAL RELATIVITY

Part 1

Kuna stori ambayo haina ushahidi Sana kwamba Isaac newton alidondokewa na apple na kisha akaanza kujiuliza kwanini apple lisiende juu kushoto au kulia Ila likadondokea chini? Stori hii nadhani ilibuniwa na waalimu Wa kwanza kufundisha habari za kani mvutano zilizoasisiwa na mwanafizikia Isaac newton na kisha kusambaa duniani kote ingawa Isaac newton either kwa namna hiyo au nyingine aliweza kuvumbua maswala ya kani mvutano

Nadhani alijiuliza tu kuwa Kama vitu vyote hudondokea juu ya uso Wa dunia lazima kutakuwa na kani inayosababisha vitu viangukie ktk uso Wa dunia basi kani hii hujulikana Kama kani ya uvutano juu ya uso Wa gimba husika(surface gravity) (inaweza ikawa mwezi, jua dunia Jupiter nk)

Na alipochunguza kazi za kina Copernicus, Galileo na Kepler ambao walithibitisha kuwa sayari zinazunguka jua, yeye Isaac newton alijiuliza Kama sayari zinazunguka jua lazima kutakuwa na kani inayozalishwa na jua inayozipelekea sayari zizunguke jua alipofanya tafiti zake na mahesabu yake aliweza kuja na nadharia iitwayo "newton's universal gravitational theory"

NEWTON'S GRAVITATIONAL THEORY nadhria hii ipo ktika pande mbili 1/ kani mvutano juu ya uso Wa gimba husika(mfano ukirusha jiwe linashuka chini ni kwasababu ya kani hii) hii inaitwa surface gravity 2/kani mvutano baina ya magimba mawili angani mfano dunia na mwezi, jua na Venus, jua na mercury, jua na sayri yoyote ile katika mfumo huu Wa jua, hii inaitwa newtons universal gravitational theory ambayo inarahisishwa na sheria iitwayo newton's universal law of gravitation ambayo inasema kuwa "magimba mawili angani huwa yanavutana kwa kani ambayo inatokana na zao la miuzito yao gawa kwa umbali baina yao kipeo cha pili"

Sasa nadhria hii iliweza kutuambia yafuatayo 1/gravitational force(kani ya uvutano) ipo katika distance yani haitegemei kitu ili isafirishwe Kama vile sumaku inavyovuta msumari ulio kando yake (action at a distance) 2/ kani hii haiathiri muda na muda unabaki vilevile kwa mtu yoyote mfano tukio lolote linalotokea angani wote tunaweza kuliona sawa 3/ kani hii haiathiri mwanga unaopita karibu ya gimba lolote angani 4/ Nafasi ya anga(space) ni Kama umbwe kwaio kani hii pia haina namna ya changamoto yoyote yenyewe inategemea zao la uzito Wa magimba gawa kwa umbali baina ya magimba husika

Nadhria hii imedumu kwa miaka mingi tangu miaka ya 1600s mpaka sasa ingawa mwaka 1915 ilitolewa nyaraka ya nadhria kuhusu ulimwengu ya mwanafizikia aitwae Albert Einstein ambae alitumia miaka 10 kuiandika kwa kufanya tafiti nyingi Mchongo ulikuwa hivi mwaka 1905 Albert Einstein aliweza kutoa nyaraka iitwayo "Special relativity theory" ambapo ndani aligusia mambo ya nafasi(space) na muda (time), uzito(mass) na nishati(energy), speed ya mwanga na kanuni ya uhusiano Wa maada(matter) na nishati(energy) kwa kanuni ya mass energy equivalence equation E=mc^2

na baada ya miaka 10 alikuja na nadhria nyingine iliyochomozea kutoka Katika nadhria hii ya kwanza ya special relativity theory ambayo iliitwa general relativity theory Ambayo alikuja kuongezea concept ya gravity ktk ndhria ya kwanza Itaendelea,.....part 2 ambapo tutajifunza kuhusu nadharia hizi mbili za Albert Einstein

Maelezo Uchambuzi Archimedes Justin

Posted on August 12, 2021 | Categories:

JE TUNAWEZAJE KUZITAMBUA SAYARI ANGANI WAKATI WA USIKU

Ufuatao ni mwongozo utakao kusaidia kutambua sayari wakati Wa usiku

1/ kwanza kabisa tambua kuwa sayari zinazoweza Kuonekana kwa macho bila msaada Wa kifaa chochote Kama telescope ni ( mercury, Venus, Mars, Jupiter na Saturn ) 2/sayari ambazo kamwe huwezi kuziona bila telescope ni uranus, Neptune na sayari mbilikimo(Pluto) 3/sayari hizo zinazoonekana huwa hazionekani zote kwa wakati mmoja huwa zintofautiana majira 4/Kama ni sayari basi mwanga wake utakuwa hauchezi chezi utakuwa umetulia tu Sasa utajuaje ipi ni ipi?

Tukianza na MERCURY Endapo utaona kagimba kadogo kana mng'ao mweupe mapema baada ya jua kuzama na kanabadili position kwa haraka siku hadi siku basi tambua hiyo ni mercury Tukija kwa Planet VENUS Endapo utaona ni Kama jiwe kubwa kubwa kidogo linalong'aa Sana kwa rangi nyeupe fulani kiasi kwamba hakuna hata nyota yoyote ya kufikia mng'ao wake iwe asubuhi kabla jua kuchomoza au jioni baada ya jua kuzama basi tambua hiyo ni Venus

MARS Endapo utaona ni Kama kanyota fulani kakubwa kidogo ukilinganisha na vyota zingine hasa za jirani yake na kana mwanga mwekundu ambao hauchezi chezi usiku kuanzia saa nne huko na kuendelea basi tambua hiyo ni mars JUPITER Endapo utaona ni Kama jiwe fulani kubwa kimtindo na linatoa mwanga Wa njano wakati Wa usiku mnene kuanzia saa nne na kuendelea basi tambua hiyo ni Jupiter SATURN hii ni sayari adimu Sana kuonekana mara ya mwisho ilionekana mwaka jana December 21 ikiwa imejipanga karibu na Jupiter Ila muonekano wake huwa ni kama sifa za mercury isipokuwa huwa inaonekana ucku mnene Ila ni nadra Sana kuiona Kwa muongozo zaidi nenda play store pakua app inaitwa "star walk 2" Nimemaliza. Nakaribisha maswali

Maelezo na Mwalimu Archimedes Justin
Posted on August 12, 2021 | Categories:

Wednesday, August 11, 2021

CHANZO CHA GRAVITY YA DUNIANI

Gravity ni Nini ??

"kani uvutano" ya gimba husika ambayo hushikilia vitu vyote vibaki katika uso Wa gimba hilo Inaweza kuwa dunia, mars, mwezi, jua, hata black hole, n.k.

Gravity hii hutokana na nini ? 1. NADHARIA YA SIR ISAAC NEWTON Kwa mujibu Wa sir Isaac newton, gravity ni kani inayotokana na uvutano baina ya gimba na kitu chochote kilicho katika uso Wa gimba hilo kwa jina jingine gravity hiyo huitwa "surface gravity" ambayo kanuni yake ni g=GM/r^2 IKUMBUKWE KWAMBA: g = gravity ya gimba husika(N/kg) G = universal gravitational constant M = uzito Wa gimba r = umbali baina ya kitu na gimba husika kuanzia kwenye kokwa la gimba husika Ila pia newton alifika mbali na kuipanua concept hiyo na kusema kuwa hata katika anga (space) kani hiyo ipo baina ya magimba mawili Hii huitwa universal gravitational force ambayo huelezewa kwa kutumia universal gravitational law ambayo nitairahisisha kwa kuandika kanuni yake F=GM1M2/r^2

F ni kani uvutano baina ya magimba mawili G ni universal gravitational constant M1 ni uzito Wa gimba la kwanza M2 ni uzito Wa gimba la 2 r ni umbali baina ya magimba hayo mawili Na kani hii ndo huwa Kati ya sayari na jua; dunia na mwezi; dunia na satellite za kutengenezwa; Nyota na supermassive black hole katika elliptical galaxies, n.k. ila tu ikumbukwe kuwa gimba lenye uzito Mdogo litakuwa likizunguka gimba lenye uzito Mkubwa. Sasa ukiangalia concept ya kwanza, kanuni yake hutokea katika kanuni ya pili na hii ni kutokana na point ambayo gimba lenye Uzito mdogo litakuwepo

MFANO: Ukirusha jiwe juu, ni wazi jiwe litakuwa linaathiriwa na kani uvutano ijulikanayo Kama surface gravity. Hii ndio itapelekea jiwe liseleleke kwenda juu kupingana na kani hiyo, pale unapolirusha juu (V=u-gt) mpaka litakapopoteza speed yake na kuwa sifuri (u=gt) kisha litaanza kushuka chini na kufika katika uso Wa dunia likiwa na speed Fulani,(v=u+gt) ila likifika chini u ni sawa na sifuri hivyo kanuni itakuwa v=gt. Mseleleko huo huitwa "acceleration due to gravity" Ambapo g haitakuwa tena N/kg bali itakuwa m/s^2 sababu kitu kinaseleleka under the influence of gravity.

Kama hapo nimeupiga mwingi, twende tuu taratibu, tutaelewa vizuri... Ila fikiria katika space huko ambako zinapelekwa satellite, Maana yake huko jiwe na dunia zinakuwa katika uvutano ambao unaelezewa na hiyo concept ya Pili ambako kani hiyo ya uvutani itakuwa katika uzani na kani ijulikanayo Kama centrifuge force ambayo ni Kama husukuma jiwe lisidondoke kwenye uso Wa dunia (kama nilivyoeleza hapo juu) sasa kani hizi mbili huzaa kani jumla iitwayo "centripetal force" ambayo ndo italifanya jiwe liizunguke dunia kama ambavyo satellite zinavyozunguka dunia. So, unapoona ISIS au satelite ingine yoyote inayoizunguka dunia, ujue dhana hii inafanya kazi vizuri.

Sasa hapo kote, tangu mwanzo mpaka tulipofikia hatujaligusa jua hata kidogo, kuona kama ndio chanzo cha gravity ya dunia maana yake kwa maelezo hayo, hakuna point inayoonesha kwamba chanzo cha gravity ya dunia kinatokana na jua. kama concept ya newton haitoshi basi tumwangalie ndugu yetu wa pili, Bw. Albert Einstein ,.....

2. NADHARIA YA ALBERT EINSTEIN Mwaka 1915 Albert Einstein alikuja na nadhadia iitwayo General relativity ambayo alitumia miaka 10 kuiandaa. Dhana hii ilikuja kunukuliwa kama maboresho ya nadharia ya Newton kuhusu gravity ambayo hapa nitaielezea kwa lugha laini na rahisi zaidi kwa sababu ni very very veeery complicated theory (ni ngumu, ngumu, ngumu sana) Yeye, Bw. Einstein anasema, "gravity ni matokeo ya mikunjo ya spacetime inayosababishwa na uzito-nishati Wa gimba husika" Maelezo hayo yanarahisishwa kwa kanuni iitwayo "Einsteins field equation" ambayo ni Rvu-1/2Rgvu +/\gvu =8πG*Tvu/C^4 Kamaliza😂😂

MAELEZO YA KANUNI YA EINSTEIN FIELD EQUATION Sasa katika upande Wa kwanza (wa hio hesabu ya kisayansi hapo juu) kabla ya sawa sawa inamaanisha mikunjo ya spacetime, wakati upande Wa Pili ni uzito-nishati Wa gimba husika. Tupo pamoja, sio? Sasa, Katika kanuni hiyo, hakuna point inayoonesha kuwa gravity ya dunia inatokana na jua,.....

Lakini, bado kuna mwingine anaweza akaona kama vile bado kuna ukakasi MIFANO MINGINE ZAIDI. Twende tuangalie sayari ambazo hazizunguki nyota,.... Kumbuka jua ni nyota iliyo karibu na dunia kuliko nyota zingine, Hili wote tunalifahamu. Na tunajua kuwa ulimwenguni kuna nyota nyingi sana, mabilioni na mabilioni ya nyota. Hivyo, hata nyota zingine zinafanana na jua katika upande Wa kujizalishia nishati ya joto na mwanga, mf. UY scuti, Proxima, etc.

Kama nyota yetu (jua) ina sayari, basi na nyota zingine zina angalau sayari moja, si ndio? Ila, kuna tafiti zilifanyika na kuonesha kuwa zipo sayari ambazo pia hazizunguki nyota yoyote ile. Yaani, zenyewe hazipo katika mfumo wowote Wa nyota. Sayari hizi huitwa "rogue planets" zinaambaa ambaa tu katika galaxy lakini sayari hizi zina kani uvutano, kama ilivyo dunia yetu (huenda ikawa kubwa au ndogo). Swali ni je, gravity ya hizo sayari itakuwa inatokana na nini ikiwa hazizunguki nyota yoyote ile? Kupata majibu ya swali hilo rudia maelezo juu (kuanzia kwa bw. Isaac Newton) mpaka kwenye concept ya Einstein

Kwa ndugu yetu, bw. Jamaal wa ( Wasafi Media ) nimesikia akisema kuwa endapo jua likizimika kwa dakika tano hivii, huku duniani mifumo yote ita-collapse na kuharibika na ndo utakuwa mwisho Wa uhai.. JIBU NI HAPANA...ila (jua) likizimika kuanzia muda Wa dakika nane na nusu hiviii 🤣🤣🤣🤣hahahaha UMBALI WA JUA NA DUNIA (Astronomical Unit) Iko hivi, umbali kutoka duniani mpaka kwenye jua ni kilomita 150 millioni, sawa na Astronomical Unit moja; na speed ya mwanga tunajua kwenye vacuum ni kilomita laki 3 hivii kwa sekunde. (300,000km/s) Sasa, ukitaka kujua muda ambao mwanga unatumia kusafiri kutoka kwenye jua hadi duniani chukua umbali gawanya kwa speed (yani kilometa million 150 gawanya kwa kilometa laki tatu kwa sekunde)

Hapo utapata dakika 8 na sekunde 33, hivyo, kama jua likizimika basi itatuchukua muda Wa dakika 8.33 kutambua kuwa jua limezima. Ila pia Dunia itaendelea na shughuli yake kama kawaida, ya kuzunguka jua kwa muda Wa dakika 8.33 kabla haijachukua njia ya ki trajectory either ikadondokee kwenye jua au irukie huko katika anga za mbali NB: Hapo sijaelezea kuhusu *Spacetime *galaxy *Astronomical unit(AU) *light time

Haya yote ni masomo marefu alafu na muda nao sio rafiki..... Lakini maelezo kuhusu mifumo ya uhai Ku collapse iko sawa sababu mimea itasimama kufanya photosynthesis ambayo hupelekea kutengenezwa kwa chakula katika form ya carbohydrates ambayo viumbe vingine herbivorous na hata omnivorous hupata carbohydrate hizo za mmea kupitia ecosystem (mtegemeano Wa viumbe hai katika mazingira) pia mimea huzalisha gesi ya oksijeni kama takataka ambayo hutumiwa na viumbe wengine akiwepo binadam kwa ajili ya respiration katika cells ambayo oksijeni ina act kama final hydrogen acceptor katika mitochondria cells ambapo huungana na kuunda maji,...

Andiko la @archimedes justin
Posted on August 11, 2021 | Categories:

Tuesday, August 10, 2021

UKUBWA WA ULIMWENGU NA YALIYOMO

UKUBWA WA UNIVERSE(ULIMWENGU) UKOJE

SEHEMU YA 1 Sayari inayofanana na Dunia yagunduliwa Wanasayansi wamegundua sayari ambayo inakaribia sana Dunia kwa mazingira na ukubwa wake na ambayo inazunguka nyota ijulikanayo kama Proxima Centauri, iliyo na mfumo unaokaribia zaidi mfumo wetu wa jua.

Sayari hiyo, ambayo kwa sasa imepewa jina 'Proxima b' inazunguka nyota hiyo katika eneo ambalo kuna uwezekano mkubwa sana wa kupatikana kwa maji. Proxima inapatikana umbali wa kilomita trilioni 40 na inaweza kumchukua mtu, akitumia teknolojia ya sasa ya vyombo vya usafiri wa anga za juu, maelfu ya miaka kufika huko.Kwa hesabu ya haraka chombo cha Apollo kilichotua mwezini kilikuwa kinakwenda kwa speed ya kilomita 40,000 kwa lisaa limoja kwa maana hiyo ukipiga hesabu kwa umbali huo u assume chombo hicho kwenda kwenye nyota ya proxima kiende kwa speed hiyo ya Apollo itachukua miaka 115,740 kufika huko.

Licha ya kwamba ni mbali sana, kugunduliwa kwa sayari hiyo huenda kukasisimua hisia na mawazo ya binadamu na wanasayansi kuhusu kuwepo kwa viumbe katika sayari nyingine au uwezekano wa wakati mmoja watu kuishi kwenye sayari nyingine. "Kusema kweli, kufika huko kwa sasa hiyo ni kama hadithi ya kubuni kisayansi, lakini watu sasa wanalifikiria hilo na si jambo lisiloweza kufikirika kwamba wakati mmoja huenda watu wakatuma chombo huko.

Mapema mwaka huu, bilionea Yuri Milner alisema atawekeza $100m katika utafiti wa kuunda chombo au kifaa kidogo kinachoweza kusafiri anga za juu kwa kutumia teknolojia ya laser.Chombo kama hicho kinaweza kusafiri kwa pengine asilimia 20 ya kasi ya mwanga na hivyo kufupisha safari ya kufika kwenye nyota kama vile Proxima Centauri kutoka maelfu ya miaka hadi miongo kadha.Hapa ukichukua speed ya mwanga ambayo ni kilomita bilioni 1.07 kwa lisaa limoja ukatafuta asilimia 20% yake ukapiga hesabu utakuja kuona kuwa hicho chombo kwa technologia ya laser kitachukua miaka 22 kufika huko yaani miongo miwili na miaka miwili Ugunduzi wa sayari hiyo ulifanikishwa kupitia darubini ya kisasa yenye kifaa kujulikanacho kama HARPS.Darubini hiyo imewekwa nchini Chile.

Takwimu kutoka kwa darubini hiyo zinaonyesha uzito wa Proxima b huenda ukawa mara 1.3 zaidi ya uzito wa dunia na kwamba inazunguka nyota ya Proxima katika umbali wa kilomita milioni 7.5. Huchukua siku 11.2 kumaliza mzunguko mmoja. Umbali kutoka kwa nyota hiyo na sayari hiyo ni mfupi ukilinganisha na umbali kutoka kwa Dunia hadi kwa Jua (kilomita 149 milioni). Lakini Proxima Centauri ni 'nyota nyekundu mbilikimo'. Si kubwa sana na nguvu zake si nyingi kama za Jua hivyo safari inaweza kuwa karibu na nyota hiyo lakini iwe na mazingira sawa na ya dunia.

Posted on August 10, 2021 | Categories: