Thursday, August 12, 2021

UKUBWA WA ULIMWENGU NA YALIYOMO

Mars pengine ndio sayari maarufu kuliko zote kwenye solar system pamoja na kwamba iko mbali lakini inatoa viashiria vya uwepo wa maisha hapo zamani miaka mabilioni iliyopita.

Wanasayansi kutokakna na viashiria nilivyotaja huko nyuma wanajaribu kuangalia ni kwanini maisha kwenye Mars hayapo lakini yakawepo kwenye dunia yetu na je kilichosababisha nini maisha yakatoweka.Hii itatupa picha na sisi dunia yetu hapo baadae pengine maisha hayatakuwepo. Mariner 4 ya Marekani ilikuwa ndio probe ya kwanza kutembelea Mars.Hii ilikuwa ni mission ya kuivinjari tu Mars kwa maana rahisi ni kuwa ilikwenda tu na kuchukua picha za sayari hiyo. Picha hizi ndio zilikuwa picha za kwanza kabisa kupigwa karibu .Hizo picha ziliwakatisha tamaa sana wanasayansi kwa kugundua hakuna mifereji kama ya kupitisha maji bali waliona maelfu ya craters kama ilivyo kwenye mwezi.

Miaka minne baade baada ya binadamu wa kwanza kukanyaga ardhi ya mwezi , Mariner 6 na 7 zilipiga picha zingine. Zilifanana na zile zilizopigwa na Mariner 4. Tena wanasayansi walikata tamaa kwa kugundua sayari ni sayari mfu kuliko walivyodhania. Mariner 9 mwaka 1971-1972 iliweka kwenye orbit kuizunguka Mars ili kuchukua picha za ardhi yote ya Mars kwa ujumla wake.Ingawaje muda inapiga hizo picha Mars ilifunikwa na kimbunga cha vumbi maana yake ni kwamba sehemu ya ardhi yake haikuonekana vizuri.Mwishoni mwa mission hiyo vilele vinne vilionekana juu ya mawingu ya vumbi hilo.Hivyo vilele vilikuja kuonekana ni volcano.Hii ilikuwa ni dalili njema kwao ya

kuonyesha kuwa kwenye Mars kuna maisha ya ki jiolojia ya kuweza kufanya utafiti. Volcano kubwa kuonekana na chombo cha Mariner 9 pia ndio volcano kubwa kuliko zote katika mfumo wa jua.Inaitwa Olympus Mons na ni ndefu kwenda juu mara tatu ya mlima mrefu kuliko yote duniani wa Everest ina urefu wa kilometa 27 kwenda juu nilishaelezea huko nyuma. Pia kulionekana uwanda wa lava uliosababishwa na volcano hizo,Pia kulionekana magema na mifereji ambapo hapo zama za kale maji yalipita.Uwepo wa volcano inaonyesha kuwa hapo zama za kale Mars ilikuwa na kiini cha moto kama ilivyo dunia yetu. Lakini swali linakuja je sayari hiyo bado ina kile kiini cha moto? Je volcano hiyo inaweza kulipuka? Wamarekani mwaka 1975, walirusha vyombo vinaitwa Viking probes.Hizi probe ndio zilishuka kwenye sayari hiyo kwa ajili ya kupiga picha ardhi ya Mars na kupima kama chini ya kiini chake kuna mtetemeko wowote kuonyesha kwamba kuna uwezekano wowote wa mlipuko wa volcano.Viking 1 ilipiga picha za kwanza nzuri kuonyesha kuwa Mars ni sayari jangwa yenye miamba myekundu na anga lake likiwa la rangi ya pink.

Picha chini kwa juu inaonyesha volcano kubwa kuliko zote kwenye solar system inaitwa Olympus Mons hiyo inaonekana kama ndogo lakini ukweli ni kwamba ina kimo cha kilomita 27 na safu ya mlima kwa umbali wa kilomita 600 kwa upana.Picha hii imepigwa na chombo cha Hope kilichorushwa na umoja wa falme za kiarabu UAE tarehe 26 february 2021 na kutua sayari ya Mars

Maelezo na Daudi Mbaga

0 comments:

Post a Comment