Thursday, August 12, 2021

JE TUNAWEZAJE KUZITAMBUA SAYARI ANGANI WAKATI WA USIKU

Ufuatao ni mwongozo utakao kusaidia kutambua sayari wakati Wa usiku

1/ kwanza kabisa tambua kuwa sayari zinazoweza Kuonekana kwa macho bila msaada Wa kifaa chochote Kama telescope ni ( mercury, Venus, Mars, Jupiter na Saturn ) 2/sayari ambazo kamwe huwezi kuziona bila telescope ni uranus, Neptune na sayari mbilikimo(Pluto) 3/sayari hizo zinazoonekana huwa hazionekani zote kwa wakati mmoja huwa zintofautiana majira 4/Kama ni sayari basi mwanga wake utakuwa hauchezi chezi utakuwa umetulia tu Sasa utajuaje ipi ni ipi?

Tukianza na MERCURY Endapo utaona kagimba kadogo kana mng'ao mweupe mapema baada ya jua kuzama na kanabadili position kwa haraka siku hadi siku basi tambua hiyo ni mercury Tukija kwa Planet VENUS Endapo utaona ni Kama jiwe kubwa kubwa kidogo linalong'aa Sana kwa rangi nyeupe fulani kiasi kwamba hakuna hata nyota yoyote ya kufikia mng'ao wake iwe asubuhi kabla jua kuchomoza au jioni baada ya jua kuzama basi tambua hiyo ni Venus

MARS Endapo utaona ni Kama kanyota fulani kakubwa kidogo ukilinganisha na vyota zingine hasa za jirani yake na kana mwanga mwekundu ambao hauchezi chezi usiku kuanzia saa nne huko na kuendelea basi tambua hiyo ni mars JUPITER Endapo utaona ni Kama jiwe fulani kubwa kimtindo na linatoa mwanga Wa njano wakati Wa usiku mnene kuanzia saa nne na kuendelea basi tambua hiyo ni Jupiter SATURN hii ni sayari adimu Sana kuonekana mara ya mwisho ilionekana mwaka jana December 21 ikiwa imejipanga karibu na Jupiter Ila muonekano wake huwa ni kama sifa za mercury isipokuwa huwa inaonekana ucku mnene Ila ni nadra Sana kuiona Kwa muongozo zaidi nenda play store pakua app inaitwa "star walk 2" Nimemaliza. Nakaribisha maswali

Maelezo na Mwalimu Archimedes Justin

0 comments:

Post a Comment