Thursday, August 12, 2021

FAHAMU INTERNET INAPATIKANAJE KWENYE ISS

INTERNET KWENYE ISS

Umewahi kufanya screen mirroring kwenye laptop na laptop au Tv, au simu na simu - yaani kufanya kinachonekana kwenye screen hii ndio kionekane kwenye screen yingine? Kwa yeyote aliyewahi kufanya hivyo hata kwa simu basi simu kichwani kwake itamjia kumbukumbu ya Airplay - kama ni mdau wa Apple. Au chrome cast, team viewer na nk - kama ni mdau wa Android. Sasa hii screen mirroring inahusikaje hapa na wakati sisu tunataka kujua kuhusu internet kwenye ISS..?

Well, internet kwenye ISS sio direct kama kwenye smartphone au laptop yako - namaanisha laptops na tablet ndani ya ISS zimefanyiwa screen mirroring na laptops nyingine huku duniani.

Hivyo basi jamaa kule ndani ya ISS anaposhika laptop au tablet na kuingia mtandaoni labda Facebook, akawa anapitia-pitia post za ipuli boi na labda labda akaipenda post yangu kuhusu na aka-comment "safi mdogo wangu"😁 Kiuhalisia ile tablet au laptop aliyoshika sio ambayo imeingia FB na kutuma hiyo comment kwenye servers za Facebook. Au kwa lugha rahisi niseme sio ambayo yenye bando (japo sio sahihi sana kusema hivi). Itakayotuma hiyo comment ni laptop iliyoko huku duniani - ambayo kimsingi imefanyiwa screen mirroring na ile ya kwenye ISS.

Kwahiyo mchakato utakuwa hivi - comment ya jamaa itaenda kwenye LAN sever (Local access network) ndani ya ISS, kisha itapelekwa kwenye Ku band antenna - ambayo iko upande wa unaongaliana na space.

Hii antenna itaisafirisha hiyo comment mpaka kwenye TDRSS (tracking and data relay satellite system) - ambazo zipo kilomita 35000+ huko. Sasa hizi satellites ndio hutuma signals huku duniani sasa - comment ndio inakuja hivyo.

Signals hupokelewa na ma-dish yaliopo pale mjini new Mexico. Baada ya kupokelewa comment ya jamaa itaingia kwenye NISN network na kuelekea kwenye mission control center - hapa mission control center sasa ndio kuna laptops zimefanyiwa mirroring na za kwenye ISS. Ikifika kwenye laptop iliyofanyiwa screen mirroring - mchakato mmoja unakuwa umeisha, unaanza wa pili. Laptop ya hapo control center ndio huingia internet kama laptop nyingine au kama simu yako tu.

Namaanisha kupitia network provider (mfano. Tigo) kuelekea kwenye servers za Facebook. Na jibu linapotoka kwenye server za Facebook hupitia mlolongo huo huo - kinyume chake kurudi kwenye ISS. Computers za pale mission control center na computers zote za NASA zipo restricted na idara ya Usalama ya IT, na website zisizohusiana na kazi zimeblokiwa hivyo wanaanga hawaulizani 'una-download au unaangaliaGa humo humo'😁

Maelezo na Ipuli

0 comments:

Post a Comment