FAHAMU MAANA YA KIPIMO CHA MIAKA YA MWANGA
Iwe ni mwanga wa laser, tochi, umeme, kibatari au mshumaa, Mwanga ni mwanga. By thay way, tukitumia makadirio.... Hipo hivi.
Kwa sekunde mwanga unasafiri kilomita laki 3. (300,000km/s) Tuanze conversation... Dakika moja ina sekunde 60... Saa moja lina dakika 60... Siku moja ina saa 24... Wiki moja ina siku 7 tutumie mwezi wenye siku 30, Kwa hiyo mwezi mmoja una siku 30... Mwaka una miezi 12... Kwa hiyo tukitaka kufahamu mwaka una sekunde ngapi tutafanya kuzidisha kwa kumaainisha mmoja anamzaa mwenzake mpaka mwaka mzima ukamilike Itakuwa sekunde kwenda saa, kwenda siku, kwenda mwezi kwenda mwaka. Tutaanzia superstructure (mwaka) hadi substracture (sekunde) Kama hivi....
1×12×30×24×60×60= =31,104,000 Nilimaanisha, "mwaka 1 una miezi 12, kila mwezi una siku 30, kila siku ina saa 24, kila saa lina dakika 60, kila dakika ina sekunde 60. Jumla= 31,104,000 sekunde kwa mwaka mzima. Tuko sawa!?? Sasa twende umbali ambao mwang unausafiri kwa mwaka mzima, Tunajua Speed ya mwanga ni 300,000km/sec Tuna sec 31,104,000
So, 300,000 × 31,104,000= =9,331,200,000,000 9,331,200,000,000 Hii ni Trilioni 9, bilioniii 331, na milioni 200, Mmmh na wew isome. Kwa hiyo mwanga unatembea kilomita 9,331,200,000,000 kwa mwaka. Huoni hii inatusumbua kuisoma, sasa bora tukasema "urefu wa mwaka wa mwanga" kuliko kusema hiyo namba kubwa mno. Kwa hiyo ukisikia kuna sayari inasadikika kuwa viumbe kama binadamu wanaweza kuishi, inaitwa Kepler 10b Ipo umbali wa... "Bilioni 12 miaka ya mwanga"
Ujue iko "kilomita bilioni 12 mara hiyo namba" Hahahahhaah, tukisema ni mbali nafikiri vipi sijui, Yani ni mbali haswa, mbali. 12 bilions light years iko hivi... 12,000,000,000× 9,331,200,000,000 =111,974,400,000,000,000,000,000km Duh, tutumie standard notation =1.119744×10²³km Hiyo ndo 12 bilion light years. (Umbali ambao, kama unasafiri katika speed ya mwanga {300,000Km/s} bila kusimama (non-stop), itakuchukua miaka bilioni 12 njiani, hahahahahha ) Unaona urahisi wanasayansi waliotumia ili namba zisikuchanganye. Kumbuka Observable Universe ni 75 bilions light years.
Maelezo na cekams cekam

Ahsante Kwa elimu
ReplyDelete