Ni swali lililoulizwa na rajabu karimu huku akitaka majibu ambayo yapo kisayansi zaidi Sasa swali hilo ni gumu kidogo na itabidi niandike gazeti sababu ili tuweze kupata majibu basi lazima history ihusike, geography, ihusike, biology ihisike, chemistry ihusike na hiyo dini ambayo haitaki tuitumie hapa nayo itabidi ihusike ili tujulishane kwanini dini haitaki tuitumie hapa
Nimepata wakati mgumu katika kutafakari kwamba nianzie wapi Ila at least nitaanzia kwenye kuzaliwa kwa sayari yetu ya dunia mpaka kutokea kwa binadam nadhani hapo tutakuwa tume cover eneo kubwa na kujifunza zaidi
Sasa ktk makala hii msingi Mkubwa utaegemea katika nadharia iitwayo "organic evolution theory" ambayo ndo nadharia inayokubalika katika sayansi Ila pia tutaangazia kuhusu chimbuko la uhai in general Sasa mfumo nitakaotumia kuandika makala hii ni "mfumo rejea" nadhani wale wataalam Wa kiswahili tutakuwa pamoja (mfumo huo ni ule Wa kuchanganya mbele Kati nyuma) Sasa tukianza na asili ya uhai tunaweza kujiuliza uhai ulitoka wapi? Nini chanzo au chimbuko la uhai?
Swali hili limekuwa likiulizwa miaka nenda miaka rudi na kutafutiwa majibu ambyo mpaka sasa yapo katika nadharia 51)Special creation theory(uumbaji maalumu) Nadhria hii inasema kuwa chanzo cha uhai na kila kitu katika ulimwengu viliumbwa na nafsi kuu ya asili ijulikanayo Kama Mungu nadhaia hii inaungwa mkono na dini nyingi zikiwemo uislam na ukristo kwa imani yangu Mimi ya ukristo(nadharia hiyo inaelezewa katika kitabu cha mwanzo 1:1, injili ya yohana Mt. 1:1-18) katika bibilia takatifu tunaambiwa Mungu aliumba ulimwengu na kila kitu kwa muda Wa siku 6 na siku ya 7 akaitakasa akapumzika Mwaka 1665 askofu aliyejulikana kwa jina la James usher alijaribu kupiga hesabu kuona ni lini tukio la uumbaji lilifanyika? Alichokifanya alikuwa akijumlisha miaka ya uzao Wa yesu kurudi nyuma mpaka kuja kumkuta Adam (uzao Wa yesu umeelezewa katika injili ya mathayo Mt. 1 na kuendelea) na hivyo alikuja kugundua kuwa ulimwengu uliumbwa miaka 4004 BC na uumbaji ulianza mwezi Wa kumi tarehe 1 na kukamilika tarehe 23 ya mwezi huo Huo saa tatu kamili asubuhi, na hii ndo imepelekea waumini wengi Wa dini(hasa wasabato) waamini ulimwengu una umri Wa miaka 6000 sababu tangu yesu apae mbinguni imepita miaka 2000 + sasa ukijumlisha na ile miaka 4004 utapata miaka 6000+ lakini askofu usher anakuwa kinyume na maandiko matakatifu sababu kwa mujibu Wa mahesabu yake tunaona tukio la uumbaji limechukua siku 22 wakati bibilia inasema uumbaji ulifanyika kwa siku 6 tu
Sasa tukirudi katika sayansi tunaona kuwa sayansi inadili na "observable phenomena" Kama nilivyoelezea katika makala ya "From what is physics to the theory of everything" kuhusu mbinu tatu za kusoma sayansi ambazo ni observation, measurement na practicals sasa katika uumbaji huo hakuna mtu aliyeshuhudia tukio la uumbaji likifanyika na hapo ndipo sayansi inapotilia shaka kuhusu nadharia hii na kizuri kuhusu sayansi ni kwamba katika sayansi huwa hatujiulizi kuwa Mungu alitoka wapi sababu antambulika kama "supernatural being" sasa Kama kuna neno nature ndani maana yake swali hilo linakuwa halina maana na kingine ni kwamba sayansi haiingiliani na maswala ya kiimani japo mwanasayansi mmoja mmoja anakuwa na dini anayoiamini mfano ni Isaac newton alikuwa mkristo mmoja safi kabisa na alifanya kazi nyingi katika dini kuliko tunavyomjua katika upande Wa sayansi aliweza hadi kupiga hesabu kiama kitakuwa lini na kwa Mara ya kwanza alipata jibu kuwa kiama kitakuwa mwaka 2016 Ila aliporudia mahesabu yake alikuja kupata 2060 kwahiyo tusubiri(time no matter what will tell) ingawa katika bibilia tunaambiwa hakuna anayejua siku ya kiama hata yesu hajui isipokuwa Mungu baba tu, pia newton anweza akawa sahihi kuhusu mwaka Ila siku na saa ndo hajui (who knows?) Sasa mwanasayansi Wa kwanza kuikosoa nadharia hii ya "special creation theory" ni Aristotle ambaye alizaliwa huko ugiriki mwaka 384 BC na kufariki mwaka 322BC Huyu alipinga kwa kutumia utafiti na hivyo utafiti wake ulipelekea ipatikane nadharia ya Pili inayojulikana Kama spontenous generation theory
2)spontenous generation theory Nadharia hii inasema kuwa uhai ulitoka katika viumbe visivyo hai na alipata ushhidi huo kwa kuona chawa wanatokea endapo nguo itakuwa chafu, au nyama inaoza na kutoa funza hivyo chawa na funza ni viumbe hai ambao tutasema wametoka katika vitu visivyo hai kwani uongo? Sasa miaka ya 1600 mwanasayansi Fransisco redi alifanya utafiti kwa kuchukua nyama mbili moja akaiacha wazi na nyingine akaifunga kabisa katika mazingira ambayo sio rafiki kwa kitu chochote kugusana nacho na baada ya siku kadhaa alikuja kukuta ile nyama aliyoiacha wazi imeoza, inatoa funza na ile ambayo aliifunga vizuri alikuta haijaharibika ndipo akagundua kuwa Aristotle hakuwa sahihi na kile tulichokiona nyama kutoa funza ni kwasababu ya viumbe wadogo wadoo wasioonekana kwa macho walikuwa huwa wanajishikiza na kuozesha kitu mfano ni bacteria pia wadudu kama nzi wanaweza kuacha mayai yao hapo na yanapokuja kuanguliwa ndipo tunaona funza Sasa jaribio kama hilo lilikuja kufanywa tena na mwanasayansi Lazaro spallanzani miaka ya 1700s na kupata matokeo yale Yale mam aliyoyapata mtangulizi wake Fransisco redi Na ugunduzi huo ulipelekea tupate tekinolojia iitwayo "biotechnology"ambayo hutumiwa viwandani katika kuzalishia vitu kama pombe kwa kutumia viumbe wadogo wadogo(mfano fangasi aitwae yeast hutumika kutengenezea pombe pia hutumiwa katika kuumua maandazi katika mchakato uitwao fermentation ambapo yeast huchakata kiwango fulani cha wanga na kuunda pombe na gesi ya carbon dioxide ambayo huumua ngano na kufanya ivimbe Ila pia wengine huitumia migahawani kwa kuchanganya kwenye unga Wa ugali sababu unga wa ugali bado ni wanga na kuufanya uumuke na kutoa ugali Mkubwa hivyo inawapa faida kimtindo) Nadharia ya tatu inaitwa cosmozoan theory
3)Cosmozoan theory Nadharia hii inasema kuwa uhai ulitoka huko katika magimba mengine na kuja kufika hapa duniani kwa njia mbali mbali ikiwemo ya kushuka kwa vimondo sasa ukakasi Wa nadharia hii ni kwamba mpaka sasa hatujapata ushahidi Wa uwepo Wa viumbe hai nje ya dunia kuanzia mercury mpaka Pluto hakuna ambapo tumeona angalau kuna chembechembe za ushhidi Wa viumbe hai au hata kuonesha kuwa kulikuwaga na viumbe hai labda tusubiri majibu ya vifaa vilivyorushwa katika sayari ya mars tuone vitatupa majibu gani nadharia ya nne
4)Steady state theory Nadharia hii inasema kuwa kila kitu unachokiona katika ulimwengu ikiwemo na viumbe hai vilikuwepogo tu havina mwanzo wala nini Lakini ukakasi Wa nadharia hii ni kwamba katika kanuni ya ulimwengu iitwayo "law of causality au law of cause and effect" tunaona haiwezekani kitu kiwepo bila kuwa na chanzo chake basi huenda tukaitetea kwa kusema kuwa kuna "uncaused cause" na kubaki hapo na hivyo itaonekana Kuwa sahihi (who knows) ingawa nadharia hii kisayansi ilikuja kupingwa vikali na utafiti uliofanya na mwanadini george lematre miaka ya 1920s kutoka ubeligiji ambaye alipelekea kupatikana kwa nadharia ya "big bang"
Muendelezo wa Sehemu zinazofuata Utazikuta Kule Juu kwenye sehemu ya madaMaelezo kutoka kwa Mwana astrophysikia Ndugu Archimedes Justine.
JE BINADAMU WALITOKEA WAPI.
SEHEMU YA PILIKatika sehemu hii ya pili tutajikita zaidi kuiangazia sayansi inasemaje kufatana na mwendelezo Wa sehemu ya kwanza(ikumbukwe kuwa movie bado hijaanza hii yote ni trela) Sasa katika upande Wa sayansi tunarudi pale katika upande Wa "special creation theory" kwanza katika sehemu ya kwanza tuliona kuwa sayansi inpata ukakasi kuhusu nadharia hii kwasababu hakuna aliyeshuhudia tukio la uumbaji sio?
Lakini pia kifo cha waaminio kuhusu umri Wa ulimwengu kuwa ni miaka 6000 kilikuja mnamo miaka ya 1940s ambacho kililetwa na mwasayansi prof. Willard F Libby ambaye alikuja na ugunduzi Wa "carbon 14 isotope dating" ugunduzi huo ulimfanya apate tuzo ya Nobel Carbon 14 dating ni kipimo cha muda Wa mabaki ya viumbe walioishi miaka mingi iliyopita ili kujua waliishi lini sasa kwa vipimo vya mabaki mengi ya mifupa viliweza kuonesha kuwa viumbe wengi waliishi miaka mingi Sana iliyopita zaidi ya hiyo elfu sita mfano ni lile fuvu la mtu Wa kale lililookotwa pale Olduvai Georgi na Dr. Leakey mwaka 1954 Kama sikosei na kuonesha kuwa kiumbe hicho chenye fuvu hilo kiliishi miaka million tatu iliyopita(yani tukirudi nyuma miaka million tatu ndo tunakutana naye akiwa anaishi Kama time travel ingewezekana) Sasa carbon 14 dating inafanyaje kazi?
Tukirudi katika kemia tunajifunza kuhusu "organic compounds" kuwa karibu robo tatu ya vitu vyote duniani ni organic compound, organic compound ni jumla ya vitu vyote vyenye carbon atom ndani yake isipokuwa vitu vichache Kama carbon monoxide, carbon dioxide, hydrogen carbonate ions na carbonate ions,.... Sasa kwakuwa vitu vingi vina carbon element hapa tunaona haja ya kuiangazia carbon Kama carbon Carbon ni element ambayo inakuwa na idadi ya punje chanya(protons) 6 na electron 6 Ila tukija katika upande Wa uzito wake tunaona uzito Wa atom yoyote kwa asilimia 99 Unatokana na kiini chake ambako katika kiini huwa kuna punje chanya(protons) na punje zisizo na chaji(neutrons) sasa kwa carbon habari ya idadi ya neutrons inakua tofauti kidogo
1) kuna carbon zenye neutron 6 ambazo huunda jumla ya neutron na proton kuwa 12 sababu idadi ya proton hubaki vile vile 2)kuna carbon zenye neutron 7 na hivyo kiini chake huwa na jumla ya punje 13 3) kuna carbon zenye neutron 8 ambazo kiini chke huwa na jumla ya punje 14 Sasa aina ya kwanza ndo hupatikana kwa wingi katika ulimwengu takribani asilimia 99 na aina ya pili huchukua karibu asilimia moja yote kwahiyo aina ya tatu ipo katika ulimwengu Ila kwa kiwango kidogo Na aina zote tatu hujulikana Kama "isotopes za carbon" wakati kite do hicho cha atoms hizo Kuwa na idadi sawa ya proton huku zikitofautiana neutron huitwa "isotopy" na kwanini hutofautiana idadi ya neutron? Hiyo ni fizikia ya ndani Sana ambayo nisingependa niiangazie hapa Ila tutajifunzia kule kwenye makala ya "From what is physics to the theory of everything" Sasa hiyo aina tatu ambayo inapunje 14 ndo tunaiita carbon 14 na hii hupatikana katika viumbe hai mfano kwenye mifupa Sasa hiyo carbon 14 ni radioactive maana yake inakuwa inavunjika kuunda vipande viwili kwa kutoa punje zenye chaji hasi na kupelekea iundwe nitrogen kila baada ya miaka 5730(muda huo ambao kitu kitatumia kuvunjika vipande viwili huitwa half life) sasa hapo kuna kanuni inayotumika kukokotoa muda ambao kiumbe kiliikuwepogo miaka mingi kanuni hiyo ni N=Noe^-T(1/2)t
Katika kanuni hiyo N inamaanisha kiasi cha carbon kilichobaki No kiwango cha awali cha carbon T(1/2) ni half life t ni muda ambao hicho kiumbe kiliishigi Kwahiyo kwa kupima kiwango cha carbon 14 kichobaki katika masalia ya mifupa kisha unalinganisha na kiwango cha carbon 14 katika kiumbe kilichopo kinachofanana nae basi unaweza kuingiza katika kanuni hiyo na kukokotoa " t" hivi ndivyo carbon 14 dating inavyofanya kazi na kwa kupima masalia ya viumbe mbali mbali tumeweza kugundua kuwa dunia na ulimwengu kiujumla Una zaidi ya miaka 6000 hivyo concept hiyo ya kidini kuhusu umri Wa ulimwengu kuwa na miaka 6000 tupa nje ya dirisha Tukirudi kwenye nadharia zetu, katika sehemu ya kwanza tuliangalia nadharia nne sio? Sasa nadharia ya tano ni 5)Biochemical evolution theory Hii ni nadharia ambayo inakúbali kamiongoni mwa jamii ya wanasayansi ambayo yenyewe inasema kuwa chanzo cha uhai ni kutoka katika muunganiko Wa kemikali mbali mbali kama vile methane, ammonia, hydrogen na water vapour ambazo ziliungana by chance na kuunda amino acids ambazo ndo kiini cha viumbe hai wote
Nadhria hii ilipendekezwa miaka ya 1920s na mnamo miaka ya 1950smwanasayansi aitwae miller aliifanyia jaribio na jaribio hilo linaitwa "miller experiment" ambapo alichukua gesi ya ammonia, hydrogen, methane na water vapour akaweka katika mtungi maalumu maabara na kuupitishia "strong electric field" iliyopelekea zitokee cheche ambzo zilisababisha gesi hizo zijiunge ktk namna Fulani na kuunda amino acid ambazo kwa kupitia by chance zinaweza kuungana na element zingine kama phosphorous nk na kuunda vinasaba/genetic materials ambazo ni DNA(deoxyribonucleic acid) na RNA(ribonucleic acid) NOTE(tunaposema by chance tunamaanisha mam zari/probability mfano chukulia umempa tumbili computer atakavyokuwa anabonyeza bonyeza keyboard obviously atakuwa anaandika utumbo tu sio? Ila inaweza kutoa kama zali tu akijikuta kaandika neno moja lenye mantiki hata "Archimedes" sasa hivyo ndivyo ilivyotokea katika namna ya kupatikana kwa amino acid na safari mbele mpaka kutokea kwa viumbe hai)
Kipengele ambacho tutaenda kukijadili baada ya kufahamu hayo ni "organic evolution theory" Hiyo ni nadharia ambayo inasema kuwa viumbe vyote vimetoka sehemu moja Ila vilikuwa vikipitia mabadiliko Mdogo Mdogo kadri muda ulivyozidi kusonga mbele na hivyo kutufanya tutofautiane Sasa kabla sijaichimba hii nadharia kiundani nataka nikupe hints za ushahidi juu ya nadharia hii ili kuondoa utata ambao unaweza kujitokeza huko mbele 1)fossils remains(masalia ya viumbe hai) 2)comperative anatomy 3)cooperative physiology 4)comparative embryology 5)Number of chromosomes Kwa Leo tuishie hapo kipindi kijacho tutazidadavua kiundani hizo hints ambazo ndo ushahidi Wa organic evolution theory kisha tutaichimba organic evolution theory yenyewe
Maelezo na Archimedes Justine
JE BINADAMU WALITOKEA WAPI.
SEHEMU YA TATUKatika sehemu ya kwanza tulijifunza kuhusu maana ya "organic evolution theory" sasa Leo katika sehemu ya tatu tutaangalia ushahidi Wa kisayansi kuhusu nadharia hii ya organic evolution
1)Masalia ya viumbe hai(fossils remains) Viumbe hai vinapokufa huoza sababu vinachakatwa na viumbe wadogo wadogo Kama bacteria na kupelekea kutoa baadhi ya elements katika mfumo Wa gesi Kama carbon dioxide, ammonia, hydrogen sulphide na kupelekea tuhisi harufu Sasa kuna baadhi ya viumbe unakuta wanashindikana kuoza sababu sio woote watakaooza mfano katika maeneo yenye baridi Kali huko viumbe kuoza ni kazi kidogo sasa tukirudi nyuma miaka mingi Sana takribani million 750 tunakutana na viumbe waitwao dinosaurs ambao walikuwa katika aina mbali mbali lakini sio hao tu pia miti mingi iliyokuwepo enzi hizo ambao kwa pamoja walikufa na wengine kuoza lakini wengine hawakuoza Sasa wale ambao hawakuoza walikuwa wanatitia chini kadri muda unavyozidi kwenda(unaweza ukashuhidia hili iache nyumba yako baada ya muda mrefu hata miaka 10 utaikuta Kama kimo chake kimepungua) sababu malighafi hititia chini sasa huko chini hufunikwa na miamba tabaka(sedimentary rocks) na kadri miaka inavyokwenda ndivyo viumbe walivyokuwa wakifa na kutitia chini huku wakikandamizwa na layers za miamba tabaka na kupelekea alama za miili yao kujichora katika miamba hiyo huku composition zao zikibadilishwa na kuwa mafuta ghafi, au gesi asilia au makaa ya mawe ambayo ndo tunayachimba Leo
Sasa kwa tafiti zilizofanyika katika alama za miamba kwa kulinganisha layers kutokea ya juu na kushuka hadi chini wataalam Wa miamba na wanabiolojia wameweza kuona kuwa alama za miamba iliyoko tabaka la juu hifanana na baadhi ya viumbe hai wanaoishi Leo wakati kadri unavyoshuka chini mfanano unazidi kutofautiana kutoka tabaka moja hadi jingine sasa hapo ndipo wakapata ushahidi kwamba evolution ilitokea sababu tunaona mabadiliko ya miundo Wa alama za viumbe kulingana na layers za miamba lakini pia kwa kupima masalia ya carbon 14 elements wataalam Wa kemia na miamba wameweza kujua miaka ya zama ambazo viumbe hao waliishi
2)Comparative embryology Huu ushahidi unazungumzia mfanano Wa vijusi vya viumbe mbalibali Wana baiolojia kwa kuchunguza vijusi vya viumbe mbali mbali pale vinapokuwa vinaundwa wameona vikifanana yani kijusi cha Kobe, samaki, binadamu, simba, kangaroo kuku nk vinafanana Sasa wakajiuliza kwanini inakuwa hivyo? Bila Shaka ni ushahidi tosha kuwa zamani sisi sote tulitoka katika chimbuko moja Ila tulikuwa tukipitia mabadiliko mbali mbali kadri miaka ilivyokuwa inakwenda
3)comparative anatomy Kwanza tujue anatomy ni nini? Anatomy ni muundo Wa mfumo Wa kiumbe hai bila kuangazia kazi zake Sasa ukiangalia viumbe wengi unakuta baadhi ya structure/muundo Wa organ zao zinakuwa zinafanana fanana mfano ukiangalia moyo Wa amphibia labda tuchukulie samaki, ukalinganisha na moyo Wa reptilia mfano mjusi na ukalinganisha na moyo Wa binadamu utaona kimuundo kuna utofauti Mdogo Moyo Wa samaki una vyumba 2 Wa reptilia una vyumba 3 wakati Wa binadam Una vyumba 4 huo ni ushahidi kuwa sisi sote tulitoka sehemu moja isipokuwa tulikuwa tukipitia mabadiliko kadha Wa kadha(evolution)
4) comparative physiology Physiology ni elimu inayoangazia kazi za mifumo ya kiumbe hai Sasa hapa kuna namna mbili ¡)Analogous structure Hii inaelezea kuwa baadhi ya viumbe huwa na organs ambazo kazi zinafanana lakini huwenda zikawa zinaonekana kutoka katika vyanzo mbali mbali mfano ni popo na kuku wote wanamabawa kwa ajili ya kupaa Ila wametofautiana chimbuko hii inaonesha kuwa mazingira yalichagiza kuwapelekea wao wawe na sifa hiyo ¡¡)homologous structure Hii inaelezea kuwa baadhi ya viumbe huwa na organs zinazofanana Ila hutofautiana katika kazi mfano ni nyani na binadam wote wana miguu ya mbele Ila kwa binadam hutumia kwa ajili ya kushikia vitu wakati nyani hutumia kwa ajili ya kutembelea
5)comparative chromosomes Hii inaelezea kuwa idadi ya chromosome hufanana fanana baina ya viumbe hai mfano binadamu Ana idadi ya chromosomes 46 wakati sokwe Ana idadi ya chromosomes 48 lakini pia muundo Wa hizo chromosomes unafanana fanana baina ya viumbe hai sasa ukaribu huo unaonesha kuwa sisi sote tumetoka katika chimbuko moja isipokuwa tulikuwa tukipitia mabadiko (evolution) kadri muda ulivyosonga Sasa chromosomes ni nini? Tutakuja kulijadili siku nyingine katika movie kamili maana trela yetu ndo inaishia hapo ingawa niliwahi kugusia kidogo chromosome ni nini katika makala ya "From what is physics to the theory of everything"
Maelezo na Archimedes Justine.
JE BINADAMU ALITOKEA WAPI.
SEHEMU YA 4.
Katika sehemu ya 1 mpaka ya 3 ilikuwa ni utangulizi ili tupate picha na mwanga katika kuangazia ufumbuzi Wa swali hilo kupitia sayansi ANGALIZO: 1)Hapa mjadala upo kisayansi zaidi, concepts zote za nadharia ya chimbuko la uhai tumeziangazia ktk makala zilizopita kwa nadharia zote 5 ikiwemo ya uumbaji maalum ambayo ilizua mjadala mrefu 2)Kama wewe unaamini katika dini na hutaki kupokea concept za sayansi inasemaje na unahisi kama utaingia majaribuni kwa mujibu wa imani yako basi tukutakie safari njema sababu vipande vilivyobaki havikufai na unaweza ukaona kama tunakufuru, sehemu inayokufaa ni part 1, 2 na 3 kuanzia part 4 na kuendelea ni sayansi tupu 3)Nadharia itakayozungumziwa hapa kati ya zile tano tulizojifunza ni nadharia ya "biochemical evolution" tu 4)Katika sehemu ya 4 na kuendelea tutakuwa tukirejea nadharia ya "organic evolution" 5)Mfumo nitakaotumia hapa ni ule Wa rejea(mbele nyuma Kati mbele nk) Naitwa Archimedes Justin
Haya twende kazi,...... Kama tungefanikiwa kuwa na tekinolojia ya kusafiri kurudi nyuma katika muda (time travel) basi Kama tungeamua kurudi nyuma miaka billion 4.5 tukio ambalo tungeliona ni tukio la kuzaliwa kwa sayari yetu pendwa "Dunia" muda huo Wa miaka billion 4.5 tangu kuzaliwa kwa dunia mpaka kufikia sasa umegawanywa katika vipindi vikuu 4 kwa mujibu Wa tawi la geografia liitwalo "geochronology" hili ni tawi maalum la jografia linaloangazia "zama"/era mbali mbali katika dunia kulingana na vipimo vya miamba ya dunia Sasa vipindi hivyo vikuu vinne ni 1)hadean era, 2)Archean era, 3)Proterozoic era na 4)Phanerozoic era Tukianza na kipindi kimoja kimoja,
1/HADEAN ERA hiki ni kipindi ambacho kinachukua muda Kati ya 4.54 billion mpaka 4000 million iliyopita ambacho dunia ilikuwa ni kama tanuru joto la kufa mtu Katika baadhi ya vitabu na machapisho unaweza kuta umeandikiwa Kama ifuatavyo(4540-4000) Mya hiyo isikupe shida mya ni kifupisho cha "million years ago" Kwahiyo itakuwa inamanisha "range" Kati ya miaka million 4540 mpaka 4000 million years ago Sasa mwanzoni mwa kipindi hiki kulitokea mlipuko Kati kati ya wingu zito lenye gas ya hydrogen kwa wingi , huku helium ikifatia na elements zingine zingine kitaalam linaitwa "solar nebulae" Mlipuko huo ulitokeaje?
Kumbuka katika fizikia tunasema hakuna kitu chochote ambacho hakipo kwenye hali ya mwendo hivyo kila kitu kipo kwenye mwendo na hata hizo ges zilikuwa kwenye mwendo zikigongana gongana sasa migongano double double ilipelekea kuongezeka kwa nishati ya ki kinetic na hivyo kufanya kasi ya migongano iongezeke zaidi Kadri muda ulivyozidi kusonga na mwishoe ikafikia kipindi zile punje za hydrogen zilipokuwa zikigongana zikawa zinajikuta zikiungana(fusion) sasa muunganiko huo huwa ni Wa kikemikali ambao hupelekea izaliwe nishati ya joto na mwanga (nuclear fusion reaction) na hydrogen zilipokuwa zikiungana basi zilikuwa zikiunda ges ya helium sasa kilichotokea ni kwamba gesi nyingi zaidi za hydrogen zilikuwa zikivutikia kuingia katika kiini na hivyo kufanya reaction/mpambano uzidi kukolea kadri muda ulivyoenda na kufanya kiini kipanuke zaidi huku joto likiendelea kuongezeka
Sasa tunajua maada ikipata joto hutanuka sio? Na maada yenye uzito Mdogo mfano gesi husogea mbali zaidi kadri joto linavyoongezeka sio? Sasa katika lile wingu kukatokea mpasuko Wa ovyo ovyo sababu ya ongezeko la joto na kupelekea zile malighafi zenye uzito Mdogo kukimbia mbali zaidi na zile zenye uzito Mkubwa kukimbia umbali Mdogo
Lakini tunakubalina kuwa kadri maada inavyokuwa mbali na chanzo cha joto ndivyo inavyozidi kupoa sio? Basi hicho ndo kilichopelekea zile gesi zilizokimbia mbali kupoa na kuanza kuunda vitufe vidogo vidogo ambavyo vilijiunia kani uvutano "surface gravity" (hii niliielezea kqtika makala yenye kichwa kiitwacho "chanzo cha gravity ya dunia") sasa surface gravity ya vigimba hivyo zikapelekea vivute malighafi mbali mbali na kuzidi kuongezeka ukubwa mpaka kuunda sayari na ndio maana unaweza kujiuliza kwanini Jupiter, Saturn, Uranus, na Neptune ni sayari zilizoundwa kwa gesi? Jibu ndo hilo hapo juu rudia maelezo Sasa kwa kesi ya Pluto kule kwenye Ukanda wake "kuiper belt" baridi ni Kali Sana kiasi kwanza zile gas zinapoa na kubadilika kutoka gesi kwenda kimiminika na kupitiliza mpaka kuwa solid na ndio maana Pluto, Charon, makemake na vigimba vingine vyote vilivyoko katika ukanda huo ambavyo tunaviita comets ni solid
Kwa kifupi kuanzia sayari ya Jupiter mpaka Neptune tunaziita outer planets Sasa turudi huku ndani kuanzia mercury mpaka asteroid belt Ukiangalia sayari ya mercury mpak mars zote ni solid na hata asteroids zote ni solid hii ni kwasababu kipindi kile wingu(solar nebulae) inasambaratika sababu ya joto Kali zile malighafi ambazo ni nzito nzito zilishindwa kukimbia umbali mrefu hivyo zikakwamia ukanda huo nazo zikaanaza kufanya mchakato kama ambao nimeuelezea katika "outer planets" uliozipelekea ziongezeke ukubwa na uzito na hivyo kuunda sayari Kwahiyo Ku summarize maelezo yote hayo ni kwamba sayari ziliundwa kwa mchakato ujulikanao kama migongano (collision) Mwaka 2003 wanajimu Wa nchini marekani walienda angani kufanya jaribio la hiyo nadharia kwa kutumia chumvi ambayo waliiweka kwenye mfuko mweupe/transparent mpana na kwakuwa katika space gravity ya dunia ni sifuri vilevipande vya chumvi vikawa vinajiundia gravity zao na kuanza kugongana na kuunda vimanundu manundu huo ulikuwa ni ushahidi tosha kuwa sayari ziliundwa kwa kutumia mchakato huo Sasa tukija katika upande Wa dunia tunaona kuwa dunia yetu Ina satellite ya asili/mwezi je ulitokeaje?
Tukibaki katika "collision theory" inasadikika kuwa gimba lenye ukubwa Wa kama sayari ya mars lililopewa jina la "theia" liligongana na dunia yetu at a certain angle na hivyo kupunguza ukubwa wake kwa kuacha malighafi zake nyingi hapa duniani na vumbi kubwa la moto lilitimuka angani na kupelekea lipoe polepole huku likijikusanya na kuunda kagimba kadogo ambako ndo mwezi tunaouona Katika kulithibitisha hilo mnamo mwaka 1972 wanajimu Wa nchini marekani walitua mwezini na kuchukua kipande cha mwamba na kurudi nacho duniani na wataalam Wa miamba walipokipima waligundua kina madini Kama haya ya kwenye uso Wa dunia (crust) hivyo kwa jaribio hilo ilikuwa ni ushahidi tosha
Sasa katika kipindi hicho gravity ya dunia iliweza kushikiria gas mbali mbali angani mam vile hydrogen, nitrogen, carbon dioxide, noble gases na water vapour isipokuwa oxygen yenyewe ilikuwa kwa kiwango kidogo sana ila ilikuja kuundwa baadae Katika kipindi hiki cha "hadean" Hapakuwa na uhai wala dalili za uwepo Wa kiumbe hai Dunia ilikuwa ni uji Wa moto
Joto lilikuwa Kali kupita maelezo Na ndio maana kipindi hichi kimepewa jina la "hadean" lilitokana na hellish ambalo ni kivumishi cha nomino hell sasa maana ya hell ni kama kuzimu/jehanam/mahari penye joto Kali nk 2)ARCHEAN ERA tutaendelea sehemu ya 5 panapo majaaliwa
JE BINADAMU ALITOKEA WAPI.
SEHEMU YA 5
Katika sehemu ya 4 tuliona zama iitwayo "hadean" Kama bado hujaipata peruzi profile yangu,... Sasa Leo tutaangalia zama ya Pili iitwayo Archean era
2)ARCHEAN ERA
Hii ni zama ambayo inakadiliwa kuwa Kati ya kipindi cha miaka 4000 million mpaka 2500 million BC NOTE:kuna changamoto niliiopokea jana kuhusu namna ya kuandika miaka kwanini inaanzia namba kubwa inafatia ndogo? Mfano ni hapo (4000-2500million years) BC hii ni kwasababu muda Wa dunia umegawanya katika sehemu kuu mbili
1)muda uliokuwepogo kabla yesu hajazaliwa (before Christ BC) 2) muda ulioanzia yesu alipozaliwa mpaka sasa na kuendelea(anno domin AD/baada ya yesu kuzaliwa) Sasa ili uelewe ngoja nikupe mfano mwepesi Fikiria labda umbali Wa kutoka ubungo hadi mbagala ni 12 km Lakini buguruni ndo Kati Kati na umbali kutoka ubungo hadi buguruni ni kilometa 6 Sasa kwakuwa buguruni ni Kati Kati basi tuseme umbali Wa buguruni ni Kama buguruni ni km 0 Kwahiyo ubungo to buguruni itakuwa 6 km na buguruni to mbagala itakuwa 6km sio?
Sasa fikiria wewe upo mbagala alafu baby wako anakuja kutoka ubungo maana yake atakuwa Kama anaporomoka kutoka kilometa 6 kuelekea kilometa 0(ubungo) kisha aanze kupandisha tena kilometa mpaka afike mbagala ambapo atatembea kilometa zingine 6 (kutokea buguruni) sio? Sasa kumbuka tabata matumbi ipo Kati Kati ya ubungo na buguruni(3km kutoka upande wowote) Kwahiyo akifika tabata matumbi tutasema ametembea umbali Wa (6-3)km maana kaanzia ubungo(6km kutoka buguruni) kashuka hadi matumbi(3km) Si umeona inavyoleta maana?
Sasa fikiria tunazungumzia muda kwahiyo badala ya kilometa chomeka muda katika vizio vya miaka alafu umbali Wa ubungo mpaka buguruni uwe ndo BC na umbali Wa buguruni mpaka mbagala uwe ndo AD alafu buguruni ndo zama alizozaliwa yesu hivyo inasimama Kama point of reference Natumaini nitakuwa nimekujibu,.... Sasa tuendelee na makala yetu Naitwa Archimedes Justin
Napatikana kwa 0622181966WhatsApp Katika kipindi hiki cha Archean era, dunia ilipoa kwa kiwango kikubwa na kufanya ujiuji katika maeneo yote kuganda na kuunda ardhi kavu "crust" na hivyo kupelekea hata angahewa kupoa na hivyo zile "water vapours" zilianza kubadilika kutoka kwenye gaseous state na kuwa liquid state na hivyo kushuka Kama mvua na kujaza mabonde mabonde makubwa kwa madogo ambayo Leo ndo tunayaita bahari na maziwa Pia kipindi hiki cha Archean ndo kipindi ambacho viumbe hai walianza kuchomoza na viumbe hai hao ni wale "cells" Wa awali au wanaitwa "pre-existing cells" Kama cell theory inavyotuambia katika tawi la baiolojia liitwalo "cytology" Sasa cell ni nini? Cell ni kiini cha chini kabisa cha uhai ambacho ndo chimbuko la uhai Kila kiumbe hai unayemjua wewe hapa duniani ameundwa kwa cell
Inaweza kuwa cell moja au muunganiko Wa cells zaidi ya mbili Kama atakuwa kaundwa kwa cell moja basi kibaiolojia tunamwita "unicellular organism" mfano ni bacteria na Kama ameundwa kwa muunganiko Wa cell zaidi ya moja basi tunamuita "multicellular organism" mfano ndo binadam ambaye tunamuangazia alitokeaje Sasa hizo cells zina sifa gani na zilitokeaje? Cells zinasifa nyingi ingawa sifa kuu za cell ni hizi zifuatazo
1) cell lazima iwe na vinasaba/genetic materials 2)cell lazima iwe inakiminika kilichoundwa ambacho asilimia kubwa ya kimiminika hicho ni maji Kimiminika hichi tunakiita "cytoplasm" 3)cell lazima iwe na uzio wake/cell membrane Sifa zingine ni za ziada na hutofautiana kutoka cell moja hadi nyingine mfano mitochondria, plasma reticulum, vacuole, cell wall, nk Sasa cells hizo za awali zilitokeaje? Namna zivyotokea ni kwa bahati nasibu/Kama zali/probability (Hapa Kama una idea ya quantum physics utaelewa mchezo unaoitwa "quantum probability" ambao niliwahi kuuelezea katika makala iliyokuwa na kichwa kisemacho "je electron ni punje au wimbi?") Sasa katika sehemu ya Pili tulijifunza kuhusu "miller's experiment" iliyofanywa na Stanley miller miaka ya 1950s ambapo alichukua gas za methane, ammonia, hydrogen,na water vapour na kuziweka katika kifaa maalum maabara na kupitisha "electric field" ambapo mwisho Wa siku ziliungana na kuunda compound iitwayo "amino acid" ambayo amino acid ni Kama tofali za kiumbe hai chochote hivyo kwa muktadha huo tunaamini kuwa hata utokeaji Wa cells za kwanza ulitokea katika namna hiyo au kwa mchanganyo Wa namna nyingi nyingi kulingana na "probability"
Chukulia mfano umempa ngedere computer abonyeze bonyeze keyboard obviously atakachokuwa anakiandika kitakuwa ni utumbo sio? Ila kadri anavyobonyeza bonyeza anaweza kujikuta kaandika neno moja lenye maana labda tuseme neno "that" fikiria akaendelea kubonyeza bonyeza anaweza akajikuta kaandika neno "is" na akiendelea kubonyeza zaidi anaweza kujikuta kaandika neno "life" sasa fikiria maneno yote yenye maana yameungana katika mpangilio maalumu kulingana na "probability" basi itasomeka "that is life" unaona tunapata sentesi yenye maana kabisa hivyo hivyo ndivyo ilivyotokea katika mchakato Wa kutokea kwa cells za awali kulikuwa kunatokea "summation of multiple probabilistic events" ambyo ilipelekea kuzaliwe utumbo/vitu vya ovyo ovyo na vitu vya maana kama tulivyoona katika mfano Wa ngedele Sasa nikurudishe juu katika sifa ya kwanza ya cells, tumesema kuwa cells lazima ziwe na vinasaba/genetic materials je genetic materials ni nini?
Katika makala yangu ya "From what is physics to the theory of everything" part 1 niliwahi kuelezea vinasaba ni nini Ila na hapa nitakazia Vinasaba/genetic materials ni materials ambazo zimebeba sifa zote za kiumbe hai mfano hiyo rangi yako ya mwili imetokana na vinasaba ulivyonavyo Sasa kama tutasafiri na kuingia mdani ya cell(fikiria cell ni mam nyumba) basi lazima kwanza tuvuke uzio(cell membrane) tukishavuka uzio tutakutana na Maji Maji(cytoplasm) na katika eneo hilo la Maji Maji tutakutana na vitu vingi sana kama vile vacuole, chloroplast mitochondrion, plasma reticulum, cell body nk kulingana na cell tulioingia Sasa kama utakuta katika eneo hilo kuna genetic materials zinaambaa ambaa tu bila mpangilo basi cell hiyo tunaiita "prokaryotic cell" au kiumbe chenye cell hiyo tutakiita "prokaryote" mfano ni Bactria
Ila kama utakuta kuna kiini maalumu chenye uzio ndani ya hiyo cytoplasm na ndani ya kiini hicho ndo kuna genetic materials basi cell hiyo tutaiita "eukaryotic cell" na kiumbe chenye cell hiyo tutakiita "eukaryote" mfano ni binadam ambaye ndo tunamuangazia alitokeaje Sasa ebu tuziangazie sifa za genetic materials kimuundo
Kwamba tambua kuwa kuna aina mbili za genetic materials 1)DNA(deoxyribonucleic acid) nazani kwa wale mliosingiziwa mtoto mshakutana na kauli "twende tukapime DNA" sio? 2) RNA(ribonucleic acid) Sasa aina zote hizo mbili hufana kwa asilimia kubwa zote zina sifa kuu tatu 1)zina carbohydrate iitwayo "ribose sugar" 2)zina "phosphate group" 3)zina nitrogenous bases Ila utofauti wao ni kwamba DNA inaumbo ina mistari miwili mirefu, RNA Ina mstari mmoja mrefu DNA ina upungufu Wa oxygen 1 katika ribose sugar yake wakati RNA Ana ukamilifu Wa oxygen zote 5 DNA Ina compound iitwayo "thymine" katika nitrogenous bases zake wakati RNA Ina compound iitwayo Uracil badala ya thymine katika nitrogenous bases zake
Mara nyingi RNA hutengenezwa na DNA katika mchakato ujulikanao kama "DNA transcription" Sasa tuanze na moja moja kuichambua DNA Hii ni material ambayo inkuwa na umbo kama ngazi ambayo imesokotwa na kuunda nane nane zinazojirudia kulingana na urefu wake, kila nane tunaiita "DNA molecule" ambayo inakuwa na phosphate group, ribose sugar na nitrogenous base Sasa inakuwa ndefu kiasi cha kuunda burungutu kama kamba ya kufumia vitambaa sasa burungutu hilo ndo tunaliita "chromosome" Sasa fikiria unakunjulua hilo burungutu basi utakuwa na kamba ndefu sio? Sasa fikria unakata kata kamba katika vipande vipande kwa kuangalia nane nane kadhaa basi vipande hivyo ndo tunaviita "gene"ambavyo ndo hubeba sifa mbali mbali za kiumbe hai na kila kipande huwa na sifa yake ambayo hukaa katika namna ya ukinzani mfano ufupi na urefu, unene na wembamba, akili na ukilaza, weupe na weusi, nk ambapo katika kipengele za uzalianaji kwa viumbe ambao hujamiana lazima kutokee segregation katika genital epithelial cells(cells za awali za uzazi) ili kusudi sifa moja Kati ya hizo mbili ndo iende kwenye yai au sperm mchakato huo kwa jina lingine huitwa "meiosis" Sasa tukirudi pale juu niligusia nitrogenous bases ambazo pia zinaonesha utofauti Kati ya DNA na RNA Sasa nitrogenous bases ni nini?
Nitrogenous bases ni materials complex ambazo zimeundwa kwa muunganiko wa element nyingi nyingi tofauti ila kuu ni nitrogen Nitrogenous bases hizo ni Thymine, uracil,adenine, cytosine, na guanine, Sasa base hizi hushikana kwa kuendana kama ifuatavyo kwa upande Wa DNA T-A C-G hapo inaweza ikaendelea kulingana kwa mchanganyo kutokana na urefu Wa DNA structure kama ifuatavyo C-G T-A G-C A-T kikubwa tu T i match na A wakati C Ina match na G Sasa kwa upande Wa RNA utofauti Wa hizo nitrogenous bases upo kwenye Thymine Badala ya thymine kunakuwa na uracil ambayo ita match na Adenine na bases zingine zilizobaki zinaendelea kama kawaida mfano U-A C-G A-U G-C hivyo hivyo na kuendelea Sasa kumbuka nimekuambia Mara nyingi RNA inaundwa na DNA katika mchakato uitwao "DNA transcription" sasa hapo tutajiuliza je uracil inatoka wapi? Wakati katika components za DNA hatuioni? Stay connected to part 6 NOTE kuna mmoja naona alinipa ofa ya bando la internet napenda kumshukuru sana pia kama ukiguswa namba iko hapo juu Na kwa wale walioomba nifungue kundi la WhatsApp nipende kuwaomba radhi sitafanya hivyo sababu muda Wa kuratibu group sina Kwa huduma za vitabu soft copy nicheki kwenye number 0622181966whatsapp huduma ya vitabu ni bure narudia tena huduma ya vitabu ni bure kuna vitabu mbali mbali kama vile sayansi, dini,mapenzi, uchumi, saikolojia na tunaweza kuvijadili kwa pamoja endapo kunasehemu utapata utata na ndio dhumuni la hiyo namba ya WhatsApp kuwepo hapo nk Knowledge is unending adventure never stop learning





0 comments:
Post a Comment