Part 1
Kuna stori ambayo haina ushahidi Sana kwamba Isaac newton alidondokewa na apple na kisha akaanza kujiuliza kwanini apple lisiende juu kushoto au kulia Ila likadondokea chini? Stori hii nadhani ilibuniwa na waalimu Wa kwanza kufundisha habari za kani mvutano zilizoasisiwa na mwanafizikia Isaac newton na kisha kusambaa duniani kote ingawa Isaac newton either kwa namna hiyo au nyingine aliweza kuvumbua maswala ya kani mvutano
Nadhani alijiuliza tu kuwa Kama vitu vyote hudondokea juu ya uso Wa dunia lazima kutakuwa na kani inayosababisha vitu viangukie ktk uso Wa dunia basi kani hii hujulikana Kama kani ya uvutano juu ya uso Wa gimba husika(surface gravity) (inaweza ikawa mwezi, jua dunia Jupiter nk)
Na alipochunguza kazi za kina Copernicus, Galileo na Kepler ambao walithibitisha kuwa sayari zinazunguka jua, yeye Isaac newton alijiuliza Kama sayari zinazunguka jua lazima kutakuwa na kani inayozalishwa na jua inayozipelekea sayari zizunguke jua alipofanya tafiti zake na mahesabu yake aliweza kuja na nadharia iitwayo "newton's universal gravitational theory"
NEWTON'S GRAVITATIONAL THEORY nadhria hii ipo ktika pande mbili 1/ kani mvutano juu ya uso Wa gimba husika(mfano ukirusha jiwe linashuka chini ni kwasababu ya kani hii) hii inaitwa surface gravity 2/kani mvutano baina ya magimba mawili angani mfano dunia na mwezi, jua na Venus, jua na mercury, jua na sayri yoyote ile katika mfumo huu Wa jua, hii inaitwa newtons universal gravitational theory ambayo inarahisishwa na sheria iitwayo newton's universal law of gravitation ambayo inasema kuwa "magimba mawili angani huwa yanavutana kwa kani ambayo inatokana na zao la miuzito yao gawa kwa umbali baina yao kipeo cha pili"
Sasa nadhria hii iliweza kutuambia yafuatayo 1/gravitational force(kani ya uvutano) ipo katika distance yani haitegemei kitu ili isafirishwe Kama vile sumaku inavyovuta msumari ulio kando yake (action at a distance) 2/ kani hii haiathiri muda na muda unabaki vilevile kwa mtu yoyote mfano tukio lolote linalotokea angani wote tunaweza kuliona sawa 3/ kani hii haiathiri mwanga unaopita karibu ya gimba lolote angani 4/ Nafasi ya anga(space) ni Kama umbwe kwaio kani hii pia haina namna ya changamoto yoyote yenyewe inategemea zao la uzito Wa magimba gawa kwa umbali baina ya magimba husika
Nadhria hii imedumu kwa miaka mingi tangu miaka ya 1600s mpaka sasa ingawa mwaka 1915 ilitolewa nyaraka ya nadhria kuhusu ulimwengu ya mwanafizikia aitwae Albert Einstein ambae alitumia miaka 10 kuiandika kwa kufanya tafiti nyingi Mchongo ulikuwa hivi mwaka 1905 Albert Einstein aliweza kutoa nyaraka iitwayo "Special relativity theory" ambapo ndani aligusia mambo ya nafasi(space) na muda (time), uzito(mass) na nishati(energy), speed ya mwanga na kanuni ya uhusiano Wa maada(matter) na nishati(energy) kwa kanuni ya mass energy equivalence equation E=mc^2
na baada ya miaka 10 alikuja na nadhria nyingine iliyochomozea kutoka Katika nadhria hii ya kwanza ya special relativity theory ambayo iliitwa general relativity theory Ambayo alikuja kuongezea concept ya gravity ktk ndhria ya kwanza Itaendelea,.....part 2 ambapo tutajifunza kuhusu nadharia hizi mbili za Albert Einstein
Maelezo Uchambuzi Archimedes Justin

0 comments:
Post a Comment