Wednesday, August 11, 2021

CHANZO CHA GRAVITY YA DUNIANI

Gravity ni Nini ??

"kani uvutano" ya gimba husika ambayo hushikilia vitu vyote vibaki katika uso Wa gimba hilo Inaweza kuwa dunia, mars, mwezi, jua, hata black hole, n.k.

Gravity hii hutokana na nini ? 1. NADHARIA YA SIR ISAAC NEWTON Kwa mujibu Wa sir Isaac newton, gravity ni kani inayotokana na uvutano baina ya gimba na kitu chochote kilicho katika uso Wa gimba hilo kwa jina jingine gravity hiyo huitwa "surface gravity" ambayo kanuni yake ni g=GM/r^2 IKUMBUKWE KWAMBA: g = gravity ya gimba husika(N/kg) G = universal gravitational constant M = uzito Wa gimba r = umbali baina ya kitu na gimba husika kuanzia kwenye kokwa la gimba husika Ila pia newton alifika mbali na kuipanua concept hiyo na kusema kuwa hata katika anga (space) kani hiyo ipo baina ya magimba mawili Hii huitwa universal gravitational force ambayo huelezewa kwa kutumia universal gravitational law ambayo nitairahisisha kwa kuandika kanuni yake F=GM1M2/r^2

F ni kani uvutano baina ya magimba mawili G ni universal gravitational constant M1 ni uzito Wa gimba la kwanza M2 ni uzito Wa gimba la 2 r ni umbali baina ya magimba hayo mawili Na kani hii ndo huwa Kati ya sayari na jua; dunia na mwezi; dunia na satellite za kutengenezwa; Nyota na supermassive black hole katika elliptical galaxies, n.k. ila tu ikumbukwe kuwa gimba lenye uzito Mdogo litakuwa likizunguka gimba lenye uzito Mkubwa. Sasa ukiangalia concept ya kwanza, kanuni yake hutokea katika kanuni ya pili na hii ni kutokana na point ambayo gimba lenye Uzito mdogo litakuwepo

MFANO: Ukirusha jiwe juu, ni wazi jiwe litakuwa linaathiriwa na kani uvutano ijulikanayo Kama surface gravity. Hii ndio itapelekea jiwe liseleleke kwenda juu kupingana na kani hiyo, pale unapolirusha juu (V=u-gt) mpaka litakapopoteza speed yake na kuwa sifuri (u=gt) kisha litaanza kushuka chini na kufika katika uso Wa dunia likiwa na speed Fulani,(v=u+gt) ila likifika chini u ni sawa na sifuri hivyo kanuni itakuwa v=gt. Mseleleko huo huitwa "acceleration due to gravity" Ambapo g haitakuwa tena N/kg bali itakuwa m/s^2 sababu kitu kinaseleleka under the influence of gravity.

Kama hapo nimeupiga mwingi, twende tuu taratibu, tutaelewa vizuri... Ila fikiria katika space huko ambako zinapelekwa satellite, Maana yake huko jiwe na dunia zinakuwa katika uvutano ambao unaelezewa na hiyo concept ya Pili ambako kani hiyo ya uvutani itakuwa katika uzani na kani ijulikanayo Kama centrifuge force ambayo ni Kama husukuma jiwe lisidondoke kwenye uso Wa dunia (kama nilivyoeleza hapo juu) sasa kani hizi mbili huzaa kani jumla iitwayo "centripetal force" ambayo ndo italifanya jiwe liizunguke dunia kama ambavyo satellite zinavyozunguka dunia. So, unapoona ISIS au satelite ingine yoyote inayoizunguka dunia, ujue dhana hii inafanya kazi vizuri.

Sasa hapo kote, tangu mwanzo mpaka tulipofikia hatujaligusa jua hata kidogo, kuona kama ndio chanzo cha gravity ya dunia maana yake kwa maelezo hayo, hakuna point inayoonesha kwamba chanzo cha gravity ya dunia kinatokana na jua. kama concept ya newton haitoshi basi tumwangalie ndugu yetu wa pili, Bw. Albert Einstein ,.....

2. NADHARIA YA ALBERT EINSTEIN Mwaka 1915 Albert Einstein alikuja na nadhadia iitwayo General relativity ambayo alitumia miaka 10 kuiandaa. Dhana hii ilikuja kunukuliwa kama maboresho ya nadharia ya Newton kuhusu gravity ambayo hapa nitaielezea kwa lugha laini na rahisi zaidi kwa sababu ni very very veeery complicated theory (ni ngumu, ngumu, ngumu sana) Yeye, Bw. Einstein anasema, "gravity ni matokeo ya mikunjo ya spacetime inayosababishwa na uzito-nishati Wa gimba husika" Maelezo hayo yanarahisishwa kwa kanuni iitwayo "Einsteins field equation" ambayo ni Rvu-1/2Rgvu +/\gvu =8πG*Tvu/C^4 Kamaliza😂😂

MAELEZO YA KANUNI YA EINSTEIN FIELD EQUATION Sasa katika upande Wa kwanza (wa hio hesabu ya kisayansi hapo juu) kabla ya sawa sawa inamaanisha mikunjo ya spacetime, wakati upande Wa Pili ni uzito-nishati Wa gimba husika. Tupo pamoja, sio? Sasa, Katika kanuni hiyo, hakuna point inayoonesha kuwa gravity ya dunia inatokana na jua,.....

Lakini, bado kuna mwingine anaweza akaona kama vile bado kuna ukakasi MIFANO MINGINE ZAIDI. Twende tuangalie sayari ambazo hazizunguki nyota,.... Kumbuka jua ni nyota iliyo karibu na dunia kuliko nyota zingine, Hili wote tunalifahamu. Na tunajua kuwa ulimwenguni kuna nyota nyingi sana, mabilioni na mabilioni ya nyota. Hivyo, hata nyota zingine zinafanana na jua katika upande Wa kujizalishia nishati ya joto na mwanga, mf. UY scuti, Proxima, etc.

Kama nyota yetu (jua) ina sayari, basi na nyota zingine zina angalau sayari moja, si ndio? Ila, kuna tafiti zilifanyika na kuonesha kuwa zipo sayari ambazo pia hazizunguki nyota yoyote ile. Yaani, zenyewe hazipo katika mfumo wowote Wa nyota. Sayari hizi huitwa "rogue planets" zinaambaa ambaa tu katika galaxy lakini sayari hizi zina kani uvutano, kama ilivyo dunia yetu (huenda ikawa kubwa au ndogo). Swali ni je, gravity ya hizo sayari itakuwa inatokana na nini ikiwa hazizunguki nyota yoyote ile? Kupata majibu ya swali hilo rudia maelezo juu (kuanzia kwa bw. Isaac Newton) mpaka kwenye concept ya Einstein

Kwa ndugu yetu, bw. Jamaal wa ( Wasafi Media ) nimesikia akisema kuwa endapo jua likizimika kwa dakika tano hivii, huku duniani mifumo yote ita-collapse na kuharibika na ndo utakuwa mwisho Wa uhai.. JIBU NI HAPANA...ila (jua) likizimika kuanzia muda Wa dakika nane na nusu hiviii 🤣🤣🤣🤣hahahaha UMBALI WA JUA NA DUNIA (Astronomical Unit) Iko hivi, umbali kutoka duniani mpaka kwenye jua ni kilomita 150 millioni, sawa na Astronomical Unit moja; na speed ya mwanga tunajua kwenye vacuum ni kilomita laki 3 hivii kwa sekunde. (300,000km/s) Sasa, ukitaka kujua muda ambao mwanga unatumia kusafiri kutoka kwenye jua hadi duniani chukua umbali gawanya kwa speed (yani kilometa million 150 gawanya kwa kilometa laki tatu kwa sekunde)

Hapo utapata dakika 8 na sekunde 33, hivyo, kama jua likizimika basi itatuchukua muda Wa dakika 8.33 kutambua kuwa jua limezima. Ila pia Dunia itaendelea na shughuli yake kama kawaida, ya kuzunguka jua kwa muda Wa dakika 8.33 kabla haijachukua njia ya ki trajectory either ikadondokee kwenye jua au irukie huko katika anga za mbali NB: Hapo sijaelezea kuhusu *Spacetime *galaxy *Astronomical unit(AU) *light time

Haya yote ni masomo marefu alafu na muda nao sio rafiki..... Lakini maelezo kuhusu mifumo ya uhai Ku collapse iko sawa sababu mimea itasimama kufanya photosynthesis ambayo hupelekea kutengenezwa kwa chakula katika form ya carbohydrates ambayo viumbe vingine herbivorous na hata omnivorous hupata carbohydrate hizo za mmea kupitia ecosystem (mtegemeano Wa viumbe hai katika mazingira) pia mimea huzalisha gesi ya oksijeni kama takataka ambayo hutumiwa na viumbe wengine akiwepo binadam kwa ajili ya respiration katika cells ambayo oksijeni ina act kama final hydrogen acceptor katika mitochondria cells ambapo huungana na kuunda maji,...

Andiko la @archimedes justin

0 comments:

Post a Comment