HIVI JUA LINAZUNGUKA??
Jua ni nyota iliyo karibu na sisi (Dunia)Ni nyota ambayo inazungukwa na sayari takriban 8, ukiondoka Pluto ambayo kila mara inapoteza sifa zake za kuwa sayari. Muunganiko wa sayari, miezi, vimondo, asteroidi na mawe-mawe na gesi chafu za angani zinazozunguka Jua huunda mfumo wa Jua (solar system) Dunia ni sayari ya 3 ukitokea kwenye jua katika mpangilio wa sayari zinazo zunguka Jua Jua ndilo linalotoa nguvu ya nishati, na mwanga kwa aslimia 99% kwenye mfumo wake, Jua huwa na nguvu ya mvutano (Gravity) kubwa sana, kuweza kushika au kuvuta vitu vyote kwenye mfumo wake ili bila kupotea, vibaki vikilizunguka kila kimoja kwa njia yake na mwendokasi wake (speed) Jua ni miongoni mwa Nyota nyingine nyingi zilizo katika kikundi cha nyota (galaksi) kinachoitwa Milkway (Milkway galaxy) ▪️Je, Jua linazunguka? ▪️Linazunguka nini? ▪️Linazungukaje?
By the way, Jua linaaaminika kuzunguka kwenye galaxy yake, Mzunguko mmoja wa Jua huchukua miaka milioni 200 na.... Kila nyota kwenye Galaxies ipo katika motion kuzunguka kwenye galaxy. Uliwahi kujibiwa swali la kwanini Galaxies zinaunda spiral pattern?? Kwa sababu kila kitu kinazunguka.
Kama sayari zinavyozunguka jua, na Nyota zinazunguka blackhole. Moja ya blackhole yenye nguvu ambayo nyota zinazunguka inaitwa Sagittarius A, hii ni Blackhole katikati ya Milkway galaxy. Galaxies zinaonekana kama CD (Compact Disk) Disk inakuwa na band mbali mbali, ukichukulia CD ya movies tuseme zile band ndo rangi, Basi pale katikati ndo kuna hilo Blackhole, Kumaanisha nyota zinazunguka blackhole,
Chukua ile CD weka peni katikati zungusha, au vile CD inakuwa inazunguka kwenye DVD (hujawahi kuona) Basi vile feni linakuwa linazunguka, Unapata picha, eeh!!
Kuna nadharia ya kwamba nyota au pamoja na sayari na vitu vyote vinatembea kwenye 3 Dimensions. Yaani katika njia ya kuzunguka na kuhama. Kuna ile kwamba jua linahama (move) pamoja na galaxy yake. Mfano huu utakuwa unaongelea "motion in straight line" Kwamba kama Universe ina-expand basi galaxy zinaama in straight line kuelekea mbali Tutumie CD
Sasa weka CD kama 5 kwenye meza kumaanisha Galaxies, ziweke umbali wa karibu-karibu Ili kusema universe ina-expand basi zile CD zivute kuelekea mbalimbali ziachane. Unaona, Galaxies zimeenda kwenye straight line, ( lectlinear motion). Na hapo utona kuwa hakuna kuzunguka. Lakink tunavyosema kuzunguka na kuhama kwa pamoja kuna motion mbili, wakati CD inazunguka na bado hapohapo inatembea. Sasa kuelewa hii, chukua CD irushe angani ukiwa unaizungusha, huo mwendo ndo mwendo wa Galaxies kwenye space Twende kwenye ku-expand, Chukua CD 5 zote mkono mmoja, Zirushe kwa kuzizungusha,
Angalia matokeo huko mbele kila moja itachuka njia yake na kuachana, (Expansion) Lakin zilikuwa na motion 2 1: zinajizungusha 2: zinatembea zikiachana Hapo kwa kutumia galaxy, jua litakuwa linamizunguko miwili, ▪️Kuzunguka blackhole (revolution) na ▪️Kutembea na galaxy (universe expansion) Hii ni 3D, x,, y,, na z,, Basi Dunia itakuwa na motion 3, ▪️Kujizungusha ▪️Kuzunguka Jua na ▪️Kuondoka na jua kwa vile jua linaondoka na galaxy Kwa hiyo kila kitu ili kiweze kufanya movement kwa njia ya kuhama lazima kijizungushe. (Kwenye space) Kama hivi...
Chukua mpira, ukiwa umeutuliza sehemu, uuzungushe (rotation) Hautatulia lazima utaanza kutembea, Tena sio kutembea tu, ni kwenye "Curved (circular) path" Gari likiwa kwenye speed likitaka kukunja kona kwa speed lazima liwe kama linazunguka kwenye rotation, Hii inawezekana kusema jua lina rotation, japo ni kubwa hatuwezi kuligundua haraka, na kwa kuwa wanasayansi hawajajikita kufatalia jua ndo maana hawajataka kusema, Na mimi leo ninasema "Jua lina rotation, nipeni vifaa niwape Proof"" Rudisha mawazo kwenye CD ukiirusha kama tulivyosema utaona kama inakunja kona kukurudia, Hivyo ndivyo galaxy zilivyo... Hapo chini nawapa picha ya Milkway galaxy, uweze kuona "Disk bands" Jua linazunguka centre ya Milkway galaxy. Naongeza "Jua lina rotation"
Maelezo na Cekams Cekam

0 comments:
Post a Comment